Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) Dk. John Pombe Magufuli
akihutubia wakati akifunga mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC
kwenye ukumbi wa Julius Nyerere leo Jumamosi Agosti 18, 2019 jijini
Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) Dk. John Pombe Magufuli, wa pili kutoka kulia, Rais wa Namibia Hage Geingob
na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kulia pamoja na marais wengine
hawapo pichani wakisaini mkataba wa kubadilishana wafungwa kwa nchi za
SADC katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi na kushoto ni Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax.
Baadhi ya Marais wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa nchi za Afrka SADC wakijadiliana jambo wakati wa kufunga mkutano huo.
Marais wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini mwa nchi za Afrka SADC wakiwa katika mkutano huo. wakati wa kufungarasmi leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC) Dk. John Pombe Magufuli, wa pili kutoka kulia, Rais wa Namibia Hage Geingob
na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kulia pamoja na marais wengine
hawapo pichani wakipiga makofi mara baada ya kusaini mkataba wa
kubadilishana wafungwa kwa nchi za SADC katikati ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi na
kushoto ni Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC,Dr. Stergomena L. Tax.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Comred
Juma Homera akicheza ngoma ya Watatoga wakati wa ufungaji wa mkutano wa
39 wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini Mwa Afrika SADC leo.
……………………………………………………..
NA JOHN BUKUKU
Wakuu wa nchi 16 zinazounda
Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC wamesaini itifaki na
makubaliano mbalimbali kwa ajili ya kuanza utekelezaji. Ambapo Itifaki
iliyosainiwa na wakuu hao wa nchi ni Itifaki ya viwanda yenye lengo la
kuboresha mazingira ya kukuza viwanda viweze kuzalisha vya kutosha na
katika ubora unaoweza kushindana duniani.
Wakuu hao pia wamesaini Itifaki
ya kubadilishana wafungwa miongoni mwa nchi wanachama itakayowezesha
wafungwa waliohukumiwa nje ya nchi zao kwenda kutumikia kifungo ndani ya
nchi zao.
Aidha walisaini pia makubaliano
ya kurekebisha sheria za nchi zao ili kuendana na Itifaki zilizosainiwa
pamoja na makubaliano ya kusaidiana katika mambo ya uhalifu.
Itifaki hizo zimesainiwa wakati
wa kufunga mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi Kusini
mwa Afrika SADC uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam ambapo
pamoja na mambo mengine wakuu wa nchi 16 zinazounda jumuiya hiyo
wamesaini itifaki na makubaliano mbalimbali kwa ajili ya kuanza
utekelezaji.
Akizungumza katika wakati
akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC) Rais Dk John Magufuli ameisisistiza Sekretarieti ya SADC
kutumia fedha wanazopata vizuri badala ya kuishia kuzitumia katika
warsha, semina na mikutano.
Rais alipendekeza Sekretarieti
hiyo ione umuhimu wa kuanza kutumia fedha hizo katika masuala ya
maendeleo kama vile ya elimu, afya na miundombinu.
“Bajeti ya Jumuiya yetu inafikia
Dola milioni 74 lakini kituo cha afya kinagharimu Sh milioni 400 hadi
500 sawa na dola 200,000 ambazo zipo ndani ya uwezo wa sekretarieti, ”
alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia amesema katika
mkutano huo wamepitisha kauli mbiu itakayotumika mwaka mzima ambayo
inasisitiza ujenzi wa viwanda endelevu vitakavyoongeza ufanyaji biashara
na kukuza ajira.
Kauli mbiu hiyo inasema, “Maendeleo endelevu ya viwanda kuongeza ufanyaji biashara na kukuza ajira,”
Rais Magufuli amesema katika
mambo waliyoazimia wamehimizana nchi wanachama kuahkikisha zinajenga
miundombinu wezeshi ili kuweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizo
pamoja kuboresha sera za uchumi na fedha.
Aidha amesema mambo mengine
waliojadili katika mkutano huo ni ombi la nchi ya Burundi kutaka kuingia
SADC ambapo walijiridhisha kuwa bado kuna mambo ambayo hayajafanyiwa
kazi na kuagiza sekretatieti kuwapa taarifa hiyo na baadae kwenye
kuchunguza kama mambo hayo yamefanyiwa kazi.
Akizungumza kuhusu suala la
vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Zimbabwe Rais Magufuli amesema
wamekubaliana waendelee na mazungumzo na jumuiya za kimataifa ili
kuangalia namna ya kuondoa vikwazo hivyo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa
Sekretaieti ya SADC, Dk Stergomena Tax mkutano huo umekubaliana kuwa
Oktoba 25 mwaka huu itakuwa siku ya kutoa wito kwa jumuiya za kimataifa
kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment