Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia
afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha
Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa
wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya
Chamwino,Dk.Zipora Mfugale,akizungumzia kuhusu jinsi walivyojipanga
kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF
iliyoboreshwa na jinsi watakavyotoa ushauri kwa wananchi kujiunga na CHF
iliyoboreshwa
Mratibu wa Ugharamiaji wa huduma
za Afya-Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Boniphance
Richard,akisisitiza jambo kwa watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino
Ikulu walipotembelea na kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye
kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia afya
Dk. Doroth Gwajima,akitoa maelezo kwa watumishi wa kituo cha afya cha
Chamwino Ikulu (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji
huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya
Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya CHF iliyoboreshwa wananchi
waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya
kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa
huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya
Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika
kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji
huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku
akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
………………………….
Na.Alex Sonna,Chamwino
Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia
afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi wa afya kote nchini
kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja wanaotumia kadi za bima
ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha
mkononi kwanza.
Dk. Gwajima
ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo cha
afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za
afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.
Amewataka watumishi
wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili kuweza
kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.
Dk Gwajima Amewataka
watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi hizo ili
kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu wengi
waweze kujiunga.
Amesema hivi sasa
kadi za CHF iliyoboreshwa imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali
hali ambayo inamwezesha mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote
hadi ngazi ya mkoa.
Pia amewataka
watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza kuwavutia
wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya jamii.
“Kama tusipotoa
huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi nzima vitakuwa havina
maana lazima sisi kama watumishi wa afya tubadilike ili kuweza kuwavutia
wananchi kuja katika vituo vyetu kupata huduma ya afya”
“Sitaki kusikia
baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma taarifa zake au
mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma taarifa zake za
wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake ambazo zitatumika
katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo”amesema Dkt Gwajima.
Naye mganga mfawidhi
wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema kuwa wamejipa
kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF
iliyoboreshwa.
Kwa upande wake ,Meneja Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya Ally-Kebby Abdallah,amesema kuwa Azma ya Serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ambao mwananchi atatambuliwa lakini pesa anayochangia irudi kwenye kituo.
Hivyo ametoa raia kwa watumishi wa kituo cha Afya Chamwino kuwahamasisha wananchi wajiunge na CHF iliyoboreshwa kwa kushirikiana na uongozi wa sehemu husika.
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji, waratibu na wasimamizi wa CHF Iliyoboreshwa nchini mpaka kufikia hapa. Mradi wa HPSS utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania hadi hapo CHF Iliyoboreshwa itakapo wafikia Wananchi wote wasio katika sekta iliyo rasmi.

0 comments:
Post a Comment