Na.Alex Sonna,Dodoma
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA)
imewatolea uvivu wapangaji wake ambao wamekuwa sugu kwa kutolipa kodi ya
pango kwa wakati hali iliyosababisha kuwatolea vitu vyao nje kutokana
na kudai zaidi ya bil 1.5 huku wabunge wakitajwa kuhusika.
Pia wastaafu nao watakiwa kuhama
katika nyumba hizo kwani TBA wanaamini kuwa mtu akishastaafu anauwezo wa
kuwa na nyumba yake mwenyewe.
Akizungumza jana na waandishi wa
habari Kaimu Meneja Wakala wa Majengo Mkoa wa Dodoma Helman Tanguye
baada ya kufanya zoezi hilo alisema kuwa wadaiwa hao wamelimbikiza
madeni yao kwa miaka 10 sasa.
Alisema kuwa TBA imekuwa ikidai
fedha nyingi sana na hasa katika mkoa wa Dodoma kwa wafanyakazi wa
serikali na taasisi mbalimbali za serikali ambazo wamezipangisha.
“Mpaka sasa tunadai zaidi ya bil
1.5 hivyo lengo kuu la TBA ni kuwaondoa wale watu walioshindwa kulipa
kodi ya pango kwa wakati ili watu wanaohamia kutoka mikoa ya Dar es
salaam na mingineyo nao waweza kupata nafasi”alisema Tanguye.
Akizungumzia zoezi zima
walivyolianza alisema kuwa “tumelianza jana baada ya kufanya taratibu
zote za kisheria na mikataba inavyosema kwahiyo tuliwapa notes ya siku
30 badaye tukaongeza Siku 14 lakini zilivyokwisha tulichukua vyombo
ambavyo vinatambulika na mahakama ili tuweze kuwaondoa.
Alisema kampuni wanayoitumia
katika zoezi zima la kuwatolea watu vitu vyao nje ni Yono Auction Mart
ambayo wamekuwa wakiitumia mara kwa mara katika shughuli zao.
Wakati huo huo Tanguye alisema
kuwa TBA ukiacha kazi yake yakujenga nyumba lakini pia inamiliki nyumba
ambazo imewapangisha wananchi,taasisi,makampuni ,na wabunge lakini
chakushangaza watu hao wamekuwa wakikaidi kulipa hata baada ya kupewa
notes ya mwezi mmoja”
“Zoezi hili hapo awali lilifanyika
jijini Dar es salaam lakini kwa sasa limehamia jijini Dodoma ambapo
litakuwa endelevu kwa mikoa yote nchini”alisema.
Pia wapangaji amabao hawajahuisha
mikataba yao ya mwaka basi nao wanahusika kuondolewa kwani wanaonyesha
kyuwa hawana nia ya kuishi katika nyumba hizo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Afisa
miliki fredy mangala alisema kuwa mnamo juni 30 waliwasisitizia kuwa
wametoa notes hivyo wanaodaiwa waende wakalipe lakini baada ya kuona
wamekaidi agizo hilo wakaona bora kuchukua hatua hizo za kuwatolea vitu
vyao nje.
“Wale wote wanaodaiwa na waliopata
notes walipe madeni hayo kama inavyotakiwa hivyo zoezi hilo litakuwa
endelevu kwani sheria inakataza kwa mtumishi wa umma kuwa na madeni.
Alisema kuwa fedha zaidi ya
bil.1.5 ni nyingi sana kwani wangeweza kuzitumia ongeza nyumba nyingine
eneo la Nzuguni ambapo wana eneo la hekali 630.
Mangala alisema kuwa wabunge
nimiongoni mwa watu wanao daiwa hivyo wanachotakiwa ni kutekeleza
majukumu yao kama mikataba inavyosema nakusema kuwa wao kama wakala
wataendelea kutekeleza wajibu wao.
“Lakini endapo pia kuna mbunge
atafikia kiwango cha kutolewa basi itabidi atolewa ingawa kuna baadhi ya
wabunge wamekuwa wakijitokeza na kutuonesha ushirikiano”alisema.
Hata hivyo Malanga alisema kuwa
mikataba hiyo inaelezea mtumishi akistaafu,akifariki au kuhamishwa mkoa
mwingine inabidi kuachia nyumba ,hivyo katika zoezi hilo wanalolifanya
pia wanaangalia watu hao.
0 comments:
Post a Comment