Spika wa Bunge, Mhe. Job
Ndugai,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma
wakati akitoa taarifa juu ya Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 50 wa
chama cha mabunge Jumuiya ya Madola,kanda ya Afrika (CPA)
kitakachofanyika visiwani Zanzibar.
Katibu wa Bunge ambaye pia ni
Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Stephen Kagaigai,akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma
………………..
Na Debora Sanja, Bunge
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji
wa Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola, Kanda ya
Afrika (CPA) ambapo zaidi ya wageni 400 kutoka Nchi mbalimbali wanachama
wanatarajiwa kushiriki Mkutano huo.
Akizungumza na waandishi wa habari
Mjini Dodoma, Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai alisema Mkutano huo
unatarajiwa kufanyika katika Kisiwa cha Zanzibar kuanzia tarehe 31
Agosti hadi tarehe 5 Septemba mwaka huu.
Alisema ufunguzi wa mkutano huo
utafanyika tarehe 2 Septemba, 2019 ambapo mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Dkt.
Mohamed Shein, Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar.
“Wageni mbalimbali wamealikwa
ikiwemo Maspika kutoka nchi wananchama, manaibu spika, wabunge na
mabalozi kutoka nchi wanachama pamoja na maspika wengine kutoka mabara
na Kanda nyingine,” alisema.
Alisema hadi sasa mataifa zaidi ya
13 yameshathibitisha kushiriki huku mwitikio ukiwa ni mkubwa kutokana
na Mkutano huo kufanyika Tanzania hususan katika Kisiwa cha Zanzibar.
Mhe. Ndugai alisema mkutano huo
utasaidia kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na kuingiza
kipato cha fedha za kigeni na kutoa fursa kwa wanyabiashara nchini
kufanya biashara zao.
“Naomba kuwashauri wafanyabiashara
na Watanzania wenzangu kwa ujumla fursa hizi tunazozipata za kuaminiwa
na mataifa mbalimbali, tuzichangamkie, ni fursa adhimu ambazo mataifa
mengine wanazililia,” alisema.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge
ambaye pia ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika, Stephen Kagaigai alisema
maandalizi yote yanaendelea vizuri na kwamba sekratieri ya CPA ipo
tayari kuhudumia ugeni huo kwa ufanisi.
Kauli Mbiu ya Mkutano wa 50 wa CPA kwa mwaka huu ni “Bunge Mtandao kwa Ajili ys Kuwezesha Demokrasia”.
0 comments:
Post a Comment