NA Khalfan Said, Simiyu
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi WCF, kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa huo
kuanzisha kiwanda cha vifaa tiba kwa kutumia malighafi ya pamba.
Mhe.
Mtaka ametoa pongezi hizo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu
wakati alipotembelea banda la WCF linaloshiriki maonesho ya mwaka huu wa
2019 ya Nanenane.
“Mimi kama kiongozi wa serikali ya Mkoa, ninawashukuru sana WCF kama partner (washirika) wakubwa sana kwenye mkoa wetu hususan kwenye ujenzi wa kiwanda cha vifaa tiba.” Alifafanua.
Alisema
WCF kupitia Mkurugenzi Mkuu wake, Bw. Masha Mshomba na wakurugenzi
wengine wamekuwa wakishiriki wakubwa katika vikao vingi vya mkoa
vinavyohitaji washirika.
Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari site clearance imefanyika na wizara inaelekea kutangaza zabuni ili mradi uanze kutekelezwa.
Maonesho
ya Nanenane kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya yakabindi nje
kidogo ya mji wa Bariadi yamefunguliwa rasmi leo Agosti 1, 2019 na
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kaulimbiu ya mwaka huu
inasema “kilimo, Mifugo naUvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.”
Akizungumzia
ushiriki wa WCF kwenye maonesho hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko
huo Bw. Anselim Peter amesema, maonesho hayo ni fursa nzuri kwa Mfuko
kuelimisha waajiri, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kuhusu kazi na
majukumu ya Mfuko.
“Tupo
hapa ili kutoa elimu kwa wafanyakazi, elimu kwa waajiri namna gani
wanaweza kuwasilisha madai yao pale mfanyakazi anapopata madhara
kutokana na kazi ili hatimaye kupata fidia na mafao mbalimbali.” Alsiema
na kuongeza.
Amewakaribisha
wananchi wakiwemo waajiri kutoka Simiyu na mikoa jirani ya Shinyanga na
Mara kufika kwenye banda la WCF namba 13 lililo jirani na lango kuu la
kuingia viwanja vya Nyakabindi ili kupata elimu zaidi kuhusu huduma
mbalimbali zitolewazo na WCF.
“Katika
banda letu, tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za waajiri kujisajili na
Mfuko, kwani tunatambua Mkoa wa Simiyu unakuja juu katika uwekezaji wa
viwanda kwahivyo
tunategemea waajiri wapya wengi kutoka hapa.” Alisema.
tunategemea waajiri wapya wengi kutoka hapa.” Alisema.
Mhe. Mtaka akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la WCF |
Mkuu
wa Mkoa Mhe. Mtaka, akiongozana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF,M
Bw. Sebera Fulgence baada ya kutembelea banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim
Peter, (kulia), akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko kwa mwananchi
huyu aliyetembelea banda la WCF.
Afisa
Matekelezo Mwandamizi (WCF), Bw. Musa Mwambujule (kushoto),
akimuhudumia mwananchi huyu aliyetembelea banda namba 13 la WCF kwenye
viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu leo Agosti 1, 2019.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter.
0 comments:
Post a Comment