Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi kabla ya kutembelea Hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia wa Rondo pamoja na Shamba la miti la Rondo inayoosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni ziara ya kikazi katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi mara baada ya kutembelea Hifadhi ya msitu asilia wa Rondo unaosimamiwa na Wakala wa Hudum za Misitu Tanzania (TFS) ambao mara baada ya kuhifadhiwa ambao umekuwa na wanyamapori wakali kama vile tembeo na simba ambao wamekuwa wakivamia mashamba na kujeruhi wananchi mkoani Lindi, Wa kwanza ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo ambalo tembo wanaotokea katika Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu wa Rondo ambao wamekuwa wakivunja miti iliyopandwa kwenye shamba Rondo ambao baadhi ya miti hiyo imeshindwa kukua ipasavyo baada miti hiyo kuvunjwa mara kwa mara
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana baadhi ya watumishi wakati alipofika katika ofis za Hifadhi ya Mazingira asilia ya Msitu na Msitu wa Kupandwa wa Rondo ambapo amewaagiza watumishi wa Rondo wafanye kazi kwa maarifa na weledi wa hali ya juu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Mgenda akizungumza na baadhi ya watumishi wakati alipofika katika eneo la kupumzikia watalii katika Msitu wa mazingira asilia wa Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kutembelea msitu huo kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili watumishi pamoja na wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo iliyopo katika wilaya ya Lindi mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto mbele ni Mkuu wa HIfadhi ya Rondo, Richard Tarimo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa
kwenye mti wa Mwl. Julius Nyerere ambapo miaka ya 1970 alipofika katika
katika kijiji cha Rondo hilo aliomba apelekwe katika eneo unakopatikana
mti huo ambapo baada ya kufika alichukua gome la mti huo uitwao Mkufi na
kisha akaondoka na gome ;a mti huo licha ya kuwa haijulikani alikwenda
kulifafanyia nini gome hilo la mti huo ambao umekuwa kivutio kikubwa cha
utalii na watu wengi kutoka maeneo mbalimbali nchini wamekuwa wakienda
katika mti huo na kubandua magome yake na kisha kuondoka nayo.
(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
ameagiza kila Taasisi ya Uhifadhi nchini ihakikishe inaunda kikosi
maalum cha askari wanyamapori watakaokuwa wakitumika kudhibiti wanyama
wakali na waharibifu pindi wanapovamia makazi ya wananchi badala ya
kutegemea kikosi kimoja p cha Askari kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili
(KDU)
Agizo hilo amelitoa jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi
wa Shamba la miti la Rondo ikiwa ni ziara yake ya kikazi katika mkoa
wa Lindi.
Akizungumza na watumishi hao, Mhe.Kanyasu amesema kutokana na
Serikali kudhibiti ujangili kwa kiasi kikubwa wanyamapori kama vile
tembo, chui na simba wamekuwa wakitembea kila mahali kwa sababu hawana
hofu ya kuuliwa kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
Amesema hali hiyo imepelekea mazao pamoja na maisha ya wananchi kuwa hatarini hasa kwa wananchi wanaoishi karibu na Hifadhi.
Amesema licha ya wanyamapori hao kuongezeka ikiwa moja ya sababu ni
Serikali kuzuia kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi wanyama hao
wamekuwa wakipita njia zao za asili ambazo tayari zimevamiwa na hivyo
kusababisha matatizo makubwa kwa wananchi.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania ( TFS) Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Hifadhi za
Taifa( TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA)
ziwe na vikosi maalum vya askari watakaotumika kukabiliana na
wanyamapori hao wakati wanapovamia vijiji.
” Kwa sasa kukutana na kundi la tembo zaidi ya 500 katika miji ya
Butiama, Dodoma pamoja Morogoro ni jambo la kawaida, Hatuwezi kutegemea
KDU pekee lazima nguvu iongezwe” alisema Mhe.Kanyasu.
Amesema TFS ihakikishe inakuwa kikosi hicho cha Askari katika
Hifadhi za Mazingira Asilia ambako kuna wanyamapori wakali ma waharibifu
wakiwemo tembo na viboko, simba na chui.
Amesema kwa sasa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipokea
maombi mengi kwa siku kutoka kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori
wakali na waharibifu.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ametoa pole kwa wananchi wa
Kijiji cha Rondo kufuatia kifo cha kumpoteza Mwalimu wa shule ya msingi
pekee katika kijiji hicho aliyekufa baada ya kuuliwa na tembo baada
ya kumpiga picha tembo aliyekuwa akihangaika kumnasua mtoto wake
aliyekuwa amenaswa kwenye kichaka.
Aidha, Mhe.Kanyasu amezitaka Halmashauri nchini zinazopakana na
Hifadhi zihakikishe zinaajiri askari Wanyamapori watakaokuwa wakisaidia
kutoa msaada wa haraka pindi wanyamapori hao wanapovamia vijiji
Pia, Amezitaka Halmashauri ziangalie uwezekano wa kuwatumia askari
wanyamapori wa vijiji (VGS) kwa kuandaa utaratibu maalum wa kuwakabidhi
silaha pindi wanyamapori wanapovamia mashamba na makazi ya wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Mgenda amesema
kutokana na juhudi za uhifadhi unaofanywa na Mkoa huo umechangia
wanyamapori kuongezeka na kuwa huru kutembea kila mahali
Kufuatia na hali hiyo, Mhe. amemuomba Naibu Waziri huyo ahakikishe
Taasisi zake za Uhifadhi nchini zunatoa elimu kwa wananchi ili waweze
kujihami wakati wanyamapori hao wanavamia mali na makazi yao.
0 comments:
Post a Comment