Mbunge wa Viti maalum anayewakilisha
vijana Mhe Mariam Ditopile amekabidhi vitendea kazi zikiwemo Kompyuta
zenye thamani ya Shilingu Milioni mbili pamoja na fedha taslimu Shilingi
Laki Sita kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa
Dar Es Salaam.
Mhe Ditopile amekabidhi vitu hivyo wakati
wa ufunguzi was Baraza la Vijana ambapo pia aliwaasa UVCCM kujitokeza
hadharani kujibu porojo ambazo zimekua zikielekezwa kwa Chama na
Serikali.
Amewataka vijana wa CCM kuyaeneza mazuri
ambayo yamekua yakifanywa na Serikali ya Rais Magufuli bila kuona aibu
na kuwasihi kusimamia mstari katika kuijenga Tanzania ya viwanda kwa
vitendo na siyo maneno.
” Niwasiihi vijana wenzangu kuwa mstari
wa mbele kuyasema na kuyatangaza hadharani yale yote yanayofanywa na
serikali ya CCM katika kutekeleza ilani yake ya mwaka 2015 ambao ndio
msahafu unaotuongoza ndani ya miaka hii mitano.
Na tunaposema tuunge mkono juhudi za Mh
Rais Magufuli katika hizi zama za kuchapa kazi kama kauli mbiu yake
inavyosema ya hapa kazi tu wananchi nao wajue ni kazi kweli kwa sababu
hata sisi vijana tutaonekana kweli tunaitekeleza Ilani kwa kufanya
kazi,” amesema Mhe Ditopile.
Aidha amewapongeza UVCCM Dar Es Salaam
kwa kuwa waasisi wa KIJANI na kuongeza kuwa hivi sasa nchi nzima kampeni
hiyo imekua kubwa na imezidi kukiimarisha Chama hicho kuelekea uchaguzi
wa Serikali za Mitaa.
” Nawapongeza kwa kuwa waasisi wa kampeni
ya Kijani ambayo imefanikiwa, ila niwanasihi juhudi hizi kubwa
zisiishie kwenye matamasha tu bali ni lazima ziwe chachu ya kuhakikisha
ushindi mnono kwa Chama chety katika chaguzi zilizo mbele yetu,” amesema
Mhe Ditopile.
0 comments:
Post a Comment