Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoani Songwe Eliniko Mkola (aliyesimama) akizungumza na wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Songwe wakati wa kupokea taarifa ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari Mpaka Juni 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia
Jenerali Nicodemus Mwangela akiwasilisha taarifa ya ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari Mpaka Juni 2019 katika kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Songwe ambapo taarifa hiyo ilipokelewa na
kupitishwa.
………………….
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoani Songwe Eliniko Mkola amewapiga marufuku viongozi wa Chama
hicho Mkoani Songwe kutoa vitisho vya aina yoyote kwa Watumishi wa
Serikali Mkoani hapa.
Mkola ametoa marufuku hiyo jana
wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Songwe kilichoketi
kupotea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari
mpaka Juni 2019 ambapo taarifa hiyo ilipokelewa na kupitishwa.
“Liko tatizo la baadhi ya viongozi
wa chama kusikiliza maneno na kutoyafanyia uchunguzi pia Wapo baadhi ya
viongozi wa Chama hutishia viongozi wa Serikali, ni marufuku kwa
vitendo hivyo kuanzia leo” amesisitiza Mkola.
Ameongeza kuwa taasisi zote
zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo ni vema kujenga
mazoea ya kuzisoma ili viongozi wa chama na wale wa serikai kila mmoja
ajue mipaka yake ya utendaji kazi.
Mkola ametoa rai kwa viongozi wa
chama na serikali kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuujenga Mkoa wa
Songwe kwani wote wana nia moja ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana
Mkoani hapa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amesema viongozi wa serikali
waliopo hawana nia ya kuuharibu Mkoa wa Songwe hivyo viongozi wa chama
wawatumie katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Brig. Jen. Mwangela ameongeza kuwa
endapo viongozi wa chama wataona kuna mambo kwenye Mkoa au Halmashauri
zao hayaendi vizuri wawasilishe masuala hayo kwa viongozi walioko Mkoani
hapa ili yafanyiwe kazi na pia wajitahidi kuepuka misuguano isiyo ya
lazima.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa
wa Songwe David Kafulila amesema Viongozi wa chama na Serikali
wasioneane aibu kuelezana ukweli kuhusu mapungufu ya baadhi ya watendaji
wa serikali kwani kufanya hivyo maendeleo ya Mkoa yatachelewa.
0 comments:
Post a Comment