METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 29, 2019

JAFO ATAKA UWEKEZAJI UFANYIKE KWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE



****************
Na. Alex Mathias, Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amewataka  wadau kushirikiana kwa pamoja kuwekeza katika timu ya Taifa ya wanawake ili Taifa lipate heshima nyingine kubwa.
Jafo amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mashindano ya Mpira wa Pete ligi daraja la kwanza katika uwanja wa Jamhuri ambapo aliwapongeza wana michezo wanawake nchini.
“Sio kwamba nataka niwapake mafuta kwa mgongo wa chupa hapana ,leo hata timu ya wanawake inayocheza mpira wa miguu ndio timu iliyoshinda COSAFA tena ilikuwa timu mwalikwa, na ushindi wake haukuwa wa  kubahatisha waliweza kuwafunga Botswana,walimfunga mwenyeji Afrika Kusini hili sio jambo la mchezo, Tena katika nusu fainali kwenda fainali,yaani Afrika Kusini alivyofungwa na kutolewa pale ni kama timu yangu ya hapa nyumbani,kama tulivyoumizwa sisi juzi maana inauma,wengine hatukula siku ile,ndio maana tunasema timu ya wanawake mnatutoa kidedea sana”amesema Jafo.
Amesema kama wadau wote watashirikiana na kuamua kuwekeza katika timu ya Taifa ya  wanawake katika mpira wa pete anaamini Taifa litaenda kupata heshima nyingine kubwa sana.
Amewataka wadau wa michezo kuiunga mkono timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri katika michezo kwa kuwa bado kipaumbele hakijatolewa kwa timu hiyo.
“Tuna kila sababu ya kutafakari kwa mara nyingine,hata mh dc hapa alipoangalia hii forum kwamba michezo ya CHANETA Kitaifa ndio tunafungua hapa nadhani hata dc wangu alichoka kidogo,bado hatujatoa kipaumbele kwa netball, Uwekezaji unaopaswa kuwekwa kwenye timu hii sio mkubwa sana ,mimi siamini kama hapa tunataka  bilioni 1,nikiwauliza viongozi wa chaneta pesa wanayotaka sio nyingi sana katika viwango mbalimbali vya ushiriki ni pound 800 au dola 250 ni hela ndogo,na haiwezekani hela hii wadau wote Tanzania tukashindwa kuchangia na kupelekea timu yetu kushindwa kushiriki,”amesisitiza Jafo.
Ameahidi wizara yake ya TAMISEMI kuchangia sh mil 2 ili kuisaidia  CHANETA. “Singo mi natoa nusu na wewe toa nusu,kamwambie waziri mwenzangu Jafo ameshasema yeye anatoa nusu na nyie mtoe  nusu,haiwezekani timu ikashindwa kushiriki eti pound 800 dola 250 halafu sisi tupo wakati Rais ametupa dhamana kwenye nchi hii kumsaidia,mi nilifikiri dola 8,000,” ameongeza Jafo.
Amesema wao TAMISEMI ndio wanawatengeneza watu na yeye binafsi anawapenda watumishi hivyo kuahidi kuendelea kushirikiana nao ili kuiwezesha timu kwenda kushiriki vizuri.
Ametolea mfano nchi ya Marekani inayopata sifa kupitia michezo mengine kama mbio nchi,”Tusing’ang’anie football peke yake,twende tukafanye diversification yah ii michezo inawezakana netball ikatupa ujiko Afrika na duniani,”alisisitiza Jafo.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Taifa(Chaneta)Judith Ilunda alisema jumla ya timu 12 zinashiriki Ligi hiyo.
Ilunda ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa kwa mchezo huo alizitaja timu hizo kuwa ni Jeshi Stars Eagle na Smart za Jijini Dar es salaam,Jiji Arusha na Makutupora Dodoma ambazo zipo kundi A.
Aidha timu za kundi B ni JKT Bweni,Coca Cola Kwanza za Jijini Dar es salaam,Jiji na Tamisemi za Dodoma na Jiji Tanga.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com