Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan (JICA), Shinichi Kitaoka kwenye hoteli ya New Otani
iliyopo Tokyo nchini Japan, Agosti 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan
(JICA), Shinichi Kitaoka kwenye hoteli ya New Otani iliyopo Tokyo nchini
Japan, Agosti 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
.....................
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa
Japan, Shinzo Abe na kuishukuru Serikali ya Japan kwa ushirikiano
inaoutoa kwa Tanzania.
Amekutana
na kiongozi huyo leo (Jumamosi, Agosti 31, 2019) katika hoteli ya The
New Otani, Tokyo Japan. Amesema Tanzania inaheshimu uhusiano mzuri
uliopo kati yake na Japan
Mazungumzo
yao yalihusu masuala mbalimbali yakiwemo ya kidiplomasia pamoja na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa kwa ushirikiano kati ya
Japan na nchi yetu.
Waziri
Mkuu ameishukuru Japan kwa misaada mbalimbali ya maendeleo inayoitoa
nchini ambayo imesaidia katika kujenga uchumi na kuwaondolea wananchi
kero mbalimbali
Kadhalika,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na
wawekezaji hususan wenye viwanda wawekeze nchini ili washirikiane na
Watanzania kukuza uchumi.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli imedhamiria kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025
kupitia sekta ya viwanda.
“Japan
imepiga hatua kubwa katika tekinolojia hivyo naamini
kuwa wafanyabiashara na wenye viwanda kutoka Japan wakiwekeza Tanzania
wataleta tekinolojia yao pia.”
Awali,
Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Shinichi Kitaoka.
Katika
mazungumzo hayo kiongozi huyo wa JICA alisema wameridhia kuwa
wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutia saini mikataba mbalimbali
yenye lengo kuinua maisha ya watanzania na kujenga uchumi.
Waziri
Mkuu aliishukuru JICA kwa ushirikiano unaoutoa nchini likiwemo suala la
kuendelea kuwapokea wanafunzi wa Kitanzania na kuwasomesha katika
taaluma mbalimbali. Amesema Tanzania inathamini sana mchango unaotolewa
na JICA katika ujenzi wa barabara, huduma za Afya na elimu.
0 comments:
Post a Comment