Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Tarehe 8 Agosti 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019.
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwapungia mikono wananchi ishara ya kuwasalimu wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zilizofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. tarehe 8 Agosti 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, Simiyu
Serikali imesema kuwa kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini itaimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za Serikali za kurasimisha mifumo ya masoko ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu; kwa kuwaunganisha Wauzaji na Wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema hayo tarehe 8 Agosti 2019 wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za wakulima (Nanenane) zinazofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi Katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Amesema kuwa mbali na soko la bidhaa pia kuzinduliwa kwa Mfumo wa Kielektoniki wa usajili wa wakulima na mfumo wa kielekroniki wa Kusimamia Biashara (Agricultural Trade Management Information System – ATMIS) utaimarisha makusanyo ya maduhuli na tozo kwa kuhakikisha huduma zote za utoaji vibali, leseni na vyeti unafanyika kielektroniki na pia kudhibiti udanganyifu katika hati na nyaraka za huduma hizo.
Alizitaja faida zingine kuwa ni pamoja na Kuhakikisha kuwa kazi ya kumhudumia mteja inafanyika kwa wakati mara tu baada ya hatua zote za maombi ya utoaji vibali, na vyeti kumalizika na kuimarisha upatikaji wa taarifa na takwimu muhimu za uingizaji na usafirishaji mazao ya kilimo nje ya nchi na Kuondoa tatizo la nyaraka bandia ambalo huchangiwa na matumizi ya mfumo
Mhe Hasunga ameyataja maeneo maalumu ya kimkakati katika sekta ya kilimo ambacho kinafanyiwa maboresho ili kuimarisha usimamizi wa kilimo na kuwapatia Wakulima huduma kwa urahisi zaidi ambayo ni Bima ya Mazao, Ambapo wizara ya Kilimo imeanzisha mwongozo wa Bima ya Mazao kwa Wakulima ambao ukielekeza jinsi ya kujiunga, kutekeleza na kuwasilisha madai ili kumwezesha kulipwa fidia pale anapopata hasara.
Mapitio ya Sera na Sheria, Mhe Hasunga amesema kuwa Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo kuwa kilimo cha kibiashara.
“Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimali watu, matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu” Alikaririwa Mhe Hasunga
Zingine ni Mfumo wa upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo, Wizara inaendelea na zoezi la kupitia kwa kina mifumo iliyopo ya uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa mbegu, mbolea na viuatilifu. Aidha wizara inaendelea kutoa elimu kwa Wakulima ili wazalishe kulingana na mahitaji ya soko na kufanya kazi kwa karibu na Taasisi nyingine zinazohusika na masoko nchini ikiwemo TANTRADE na Soko la Bidhaa (TMX).
Sambamba na hayo amesema kuwa wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha kuwa kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) Sekta ya Uvuvi inaongeza ufugaji wa samaki wenye tija na endelevu katika mabwawa ili kuwe na uwezekano wa kuzalisha samaki wengi zaidi na kuondoa kabisa uvuvi haramu.
“Ni imani yangu kuwa kama ASDP II itatekelezwa vizuri, Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati kabla ya mwaka 2025” Alisisitiza
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment