NA
LUSUNGU HELELA-DSM
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii
imetaja idadi ya watalii walioingia
nchini kuwa imeongezeka kutoka Milioni
1.2 Mwaka 2016 hadi kufikia watalii Milioni 1.3 mwaka 2017 huku watalii kutoka
nchini Marekani wakiwa vinara.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kukua kwa kasi ya uchumi huku ikisaidiwa na ujenzi wa miundombinu ya
barabara katika hifadhi za Taifa.
Mbali na idadi hiyo,
Serikali imetaja mapato yaliyopatikana
kutokana na watalii hao kuwa yameongezeka kutoka wastani wa Dola za Kimarekani
Milioni 2.1 Mwaka 2016 hadi kufikia Dola Milioni 2.2 Mwaka 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudance Milanzi amesema taarifa ya utafiti huo
unaonesha kuwa Tanzania inazidi kufanya vizuri katika sekta ya utalii kwa vile
kila mwaka idadi ya watalii na mapato yamekuwa yakiongezeka.
Awali, Milanzi alisema
ripoti hiyo ya pamoja iliandaliwa kwa ushirikiano wa Benki Kuu
Tanzania(BOT), Tume ya Taifa ya Takwimu(NBS), Idara ya Uhamiaji Zanzibar,
Kwa mujibu wa Milanzi, ripoti hiyo iliyopatikana kutokana na
‘survey’ iliyofanywa katika njia kuu za watalii, ikiwemo viwanja vya
ndege pamoja na maeneo ya njia za mipaka ya kuingia nchini, pia imebaini idadi
kubwa ya watalii wanaoingia nchini wanatoka katika nchi za Marekani, Uingereza,
India, Uholanzi pamoja na Uswiswi.
Katika uzinduzi wa taarifa hiyo Milanzi amesema taarifa hizo
zilikusanywa kupitia viwanja
vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro(KIA), Abeid Aman
Karume(Zanzibar) pamoja na mipaka ya Namanga, Tunduma, Mtukula na kwingineko,
kwa kiasi kikubwa imechangiwa na idadi ya watalii walioingia nchini
na kutembelea fukwe pamoja wanyamapori
Alisema kimsingi ongezeko la watalii waliongia nchini, pia
limetokana na kasi ya kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini
inayofanywa na Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kupitia
mamlaka iliyopewa ya kuvitangaza vivutio hivyo, zikiwemo mbuga za wanyama,
fukwe, mlima Kilimanjaro na vinginevyo.
Aidha alisema mbali na vivutio hivyo pia siku za hivi karibuni
Tanzania imekuwa ikipata wageni wanaofika nchini kwa ajili ya kupata matibabu
katika hospitali zetu mbalimbali, ambao pamoja na huitaji wao katika masuala ya
tiba, wanapata fursa ya kufanya utalii na hivyo kuchangia ongezeko katika eneo
hilo.
Alisema ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Hifadhi za
Taifa pia kwa kiasi kikubwa kumechangia kuongeza idadi ya watalii wanaoingia
nchini, hatua aliyosema kuwa itazidi kuutangaza utalii wetu.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa
Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Deograsius Mdamu amesema kwa sasa
idara imeanza kuwekeza nguvu katika utalii wa fukwe kwa vile ni aina ya utalii
ambao unaonekana kupendwa na watalii
wengi wanaongiana nchini.
Wakati huo huo , amesema wanataraji kushirikiana na mamlaka mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Uendelezaji Uchumi(EPZA) katika
kutangaza utalii.
Aidha alitaja changamoto
mbalimbali zilizokuwa zinazowakabili watalii, ikiwemo masuala ya viza pamoja na
huduma za kifedha kupitia utaratibu kadi
maalumu, ni maoneo yanayoendelea kufanyiwa kazi na Wizara hiyo ili kuzidi
kuutangaza utali hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment