Waziri wa Nishati, Dkt
Medard Kalemani (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uwashaji
rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mwelani, Kata ya Mganza wilayani Chato,
Mkoa wa Geita. Wengine katika picha ni viongozi katika Kata hiyo.
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akigawa vifaa vya UMETA kwa
wananchi wa Kijiji cha Mwelani wilayani Chato ambacho kitawawezesha
kuunganishwa na umeme bila kuingia gharama za wiring.
Waziri wa Nishati, Dkt
Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi katika Kijiji cha
Mwelani wilayani Chato kabla ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.
Wataalam mbalimbali
kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), wakiwa katika Mkutano wa Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani na wananchi wa Kijiji cha Mwelani wilayani Chato.
…………………….
Teresia Mhagama na Hafsa Omar, Geita
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani
ameendelea kusisitiza utekelezaji wa agizo alilolitoa la wananchi
vijijini kutotozwa gharama ya nguzo pale wanahitaji kuunganishiwa umeme.
Dkt. Kalemani alisema hayo tarehe 7
Agosti, 2019, wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mwelani,
Kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita kabla ya kuwasha umeme rasmi
katika Kijiji hicho.
“ Kuna baadhi ya wananchi wanalalamika
kuwa wakienda kulipia huduma ya umeme ofisi za TANESCO au kwa
Wakandarasi, wanaambiwa kuwa walipie nguzo, hili suala nimeshalikataza
nchi nzima,” alisema Dkt Kalemani.
Vilevile Dkt. Kalemani aliagiza kuwa,
wananchi wasikataliwe kutoa malipo pale wanapotaka huduma ya umeme kwa
kisingizio cha kutokuwepo kwa vifaa kwani suala hilo limekuwa kama
kigezo cha kuwacheleweshea huduma wananchi.
Akizungumza na wananchi katika Kijiji
hicho aliwahakikishia kuwa, vitongoji vyote vinne vilivyopo kwenye Kata
hiyo vitapata umeme.
Aidha, alitoa agizo kwa Meneja wa TANESCO
Wilaya ya Chato kufungua ofisi ndogo ya TANESCO kwenye Kata ya Mganza
ili shughuli zote za kuhudumia wananchi zifanyike kwenye Kata hiyo na
hivyo kuwapunguzia umbali wa kufuata huduma.
Pia alitoa wito kwa wananchi, kulipia
umeme kwa wingi kwani itasadia kuenea haraka kwa umeme nchini na hivyo
kuchochea maendeleo ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment