Na
Rhoda James, Pwani
Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu amezindua rasmi upatikanaji wa huduma ya umeme katika
Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba na kijiji cha Hondogo Kata ya Mandela mkoa wa Pwani.
Uzinduzi huo ulifanyika
tarehe 3 Mei, 2018 katika vijiji hivyo wakati alipofanya ziara ya kukagua Mradi
wa Ujazilizi (Densification) na miradi mengine ya umeme inayotekelezwa mkoani
humo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO).
Katika ziara hiyo Naibu
Waziri Mgalu aliwaagiza watumishi wa TANESCO na REA kuhakikisha wanaunganishia
wananchi wote umeme kwa wakati ili wananchi wafaidike nishati hiyo kwa
maendeleo ya kiuchumi.
Pia aliwataka wananchi
wa Pwani kuchangamkia fursa ya mradi huo pindi umeme unapofika katika kata zao.
“Fanyeni wiring haraka katika Zahanati na
Mashuleni pia katika nyumba zenu ili muunganishiwe umeme wa REA kwa gharama ya
shilingi 27,000 tu,” alisema Mgalu.
Mgalu alisema kuwa
tayari Kaya 65 katika Kata ya Mandela zimeunganishwa na umeme na kaya nyingine
85 zimeongezwa kwa ajili ya utekelezaji.
Aliongeza kuwa, ifikapo
mwaka 2021 vijiji vyote nchini vitakuwa vimepata umeme kwa kuwa tayari Wakandarasi
wote wamekwisha idhinishiwa malipo yao na hivyo kuwataka ambao wameondoka
katika maeneo yao kurudi haraka.
Kwa upande wake, Diwani
wa Kata ya Lugoba Rehema Issa, alisema kuwa wananchi walichelewa wenyewe
kufanya wiring kutokana na sababu
mbalimbali lakini sasa watafanya haraka.
“Pia tulikuwa na tatizo
la transforma lakini sasa tumewekewa na wananchi wangu watapata umeme,”alisema
Issa.
Aidha, Diwani Issa
alisema yapo baadhi ya maeneo ambayo hayajapata umeme hivyo alitumia fursa hiyo
kumuomba Naibu Waziri Mgalu asaidie ili vijiji vipate umeme kwa wakati.
Kwa nyakati tofauti,
Mbunge wa Jimbo la Chalize Riziwani Kikwete alimshukuru Naibu Waziri Mgalu kwa
kutembelea jimbo lake na kwa kasi kubwa ya kuhakiksha wananchi wote wa Pwani
wanapata umeme kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment