KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini
(CPG) Phaustine Kasike wa kwanza kushoto akiwa ameshika matofali wakati
wa ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi huo katika Magereza ya Isanga na
Msalato yaliyopo jijini hapa (katikati) ni Mkuu wa Magereza mkoani
Dodoma Kenneth Mwambije
…………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
KAMISHNA Jenerali wa
Jeshi la Magereza nchini (CPG) Phaustine Kasike amewaagiza maofisa wa
jeshi hilo nchini kote kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais Dk John
Magufuli la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya stafu wa jeshi
hilo kupitia nguvu Kazi walionayo ili kuipunguzia mzigo Serikali.
Jeshi hilo linakabiliwa na tatizo la uhaba wa nyumba za maofisa hao katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Hayo aliyasema
wakati wa ziara ya kukagua mradi wa Ujenzi huo katika Magereza ya
Isanga na Msalato yaliyopo jijini hapa Kamishna Jenerali Kasike amesema
kuwa jumla ya nyumba 9000 zinatakiwa kwa ajili ya kumaliza changamoto
hiyo ambapo kila mkoa kupitia nguvu Kazi walionayo katika Magereza
wanatekeleza mradi huo.
Amesema kuwa upande
wa mkoa wa Dodoma zinatakiwa nyumba 340 katika gereza la Isanga lakini
hadi sasa tayari nyumba 137 zipo katika hatua ya mwisho ya Ujenzi huku
zikisalia 203 ambazo nazo zinatakiwa kukamilika ndani ya muda ili ziweze
kuanza kutumika kwa maofisa hao.
“Nawapongeza sana
maofisa wa Magereza kwa jitihada wanazofanya katika kusimamia Ujenzi huo
nimeona Dodoma wako vizuri na mikoa mingine fanyeni hivyo ili tufikie
lengo ikiwemo kutekeleza agizo la Rais,” amesema Kamishna Jenerali
Kasike.
Hata hivyo amesema
kuwa jitihada wanazofanya kupitia nguvu Kazi,wanaimani Serikali itaweka
nguvu ya ziada jambo ambalo watafanikiwa kumaliza tatizo hilo kabisa.
“Nahakika hadi sasa
tumepunguza gharama za Ujenzi ambazo Serikali ingetoa bila Jeshi hilo
kubuni mradi huo,zikikamilika gharama halisi ya ujenzi itajulikana kiasi
gani kimetumika na kipi kimeokolewa kama wangetumia wakandarasi “,
amesisitiza Kamishna Jenerali Kasike.
Akitolea mfano Gereza
la Isanga lililopo jijini hapa amesema nyumba 20 tayari msingi
imeshawekwa huku nyumba 14 zimefikia katika hatua ya lenta na sita
zilizosalia katika gereza hilo zinaendelea kujengwa.
Alisema Magereza hayo
wamefanya vizuri kwa sababu wametumia muda na nguvu Kazi iliopo
kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za maofisa
wa jeshi hilo.
Alisema kutokana na kutumia vyanzo vyao bado wanaimani watakamilisha ndani ya muda waliojiwekea.
Naye Mkuu wa Magereza
mkoani Dodoma Kenneth Mwambije alisema Jeshi hilo mkoani Dodoma wako
mstari wa mbele katika usimamizi wa mradi huo ili kutimiza lengo la
kukamilisha Ujenzi huo pamoja na kutatua changamoto ya tatizo hilo.
Mwambije alisema
lengo ni kuona idadi ya nyumba zinazotakiwa katika mkoa wa Dodoma kwenye
Magereza husika zinakamilika kwa wakati ili kurahisha ufanyaji Kazi wa
askari wa jeshi hilo.
“Tunashkuru Kamishna
Jenerali kutembelea mradi huu wa Ujenzi tutahakikisha usimamizi
unafanyika kifasaha na nyumba zitaendelea kukamilika,” alisema Mwambije.
Kwa upande wa wakuu
wa Gereza la Isanga na Msalato jijini Dodoma kwa nyakati tofauti
walimshkuru Kamishna Jenerali kwa kutembelea mradi wa Ujenzi na
kumuhakikishia wataendelea kusimamia ili kuhakikisha nyumba hizo
zinakamilika kwa wakati.
Huruma Mwalije ambaye ni Mkuu wa gereza la Msalato alisema lengo lao ni kuona idadi ya nyumba walizopangiwa zinakamilika.
Kwa upande wa Mkuu wa
gereza la Isanga John Daud alisema Kamishna asiwe na wasiwasi Kazi
aliyowakabidhi itafanyika kwa mujibu wa sheria Na maelekezo waliopewa.
0 comments:
Post a Comment