METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 20, 2019

FURSA YA MAFUNZO KAZINI WILAYA YA IRINGA YAKUTANISHA ZAIDI YA WASOMI 514

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wasomi waliojitokeza ofisini kwake kwa ajili ya kuchangamkia fursa ya mafunzo kanzini inayotewa na serikari ya awamu ya tano
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Zaidi ya wasomi mia tano na
kumi na nne (514) wamejitokeza katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Iringa kuchangamkia
fursa iliyotolewa na serikali ya kuwasaidia wasomi kupata mafunzo kazini kwa
mwaka mmoja na serikali itagharamia mafunzo hayo kwa kutoa kiasi cha shilingi
laki moja na nusu kila mwenzi.
 
Akizungumza na blog hii Mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano
inayongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imetenga fedha za kuwasaidia wasomi
zaidi ya elfu tano nchi nzima kufanya kazi kwenye taasisi binafsi
 
“Mheshimiwa Rais ametanga fedha
kupitia mfuko wa waziri mkuu kwa ajili ya kuwasaidia wasomi kufanya kazi kwenye
mashirika binafsi kwa lengo la kuwasaidia kupata uzoefu kazini ili wakifanya
vizuri waweze kusaidiwa na wengine kupata uzoefu ili wakienda kuomba kazi
sehemu nyingine wawe na uzoefu” alisema Kasesela
 
Kasesela alisema kuwa
alichokifanya ni kutimiza  ndoto ya Rais
Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wasomi wote wanakuwa na uzoefu kazini kwa
kuwawezesha ili kuwarahisisha kupata ajira pale wanapoenda kuomba kazi kwa kuwa
watakuwa tayari wameshafanya kazi kwenye taasisi binafsi kwa mwaka mmoja.
 
“Ukiangalia Tanzania kada moja
tu ya udaktari ndio kata ambayo imekuwa ikipewa mafunzo ya uzoefu kazini hivyo
kada nyingine zote hazina mafunzo kazini ndio maana sisi wasaidizi wake
tumeanza kutekeleza hili swala kwa nguvu zote” alisema Kasesela
 
Kasesela alisema kuwa aliitisha
zoezi hilo huku akitegemea kuwa angepata wasomi wapatao mia moja tu lakini
amekutana na wasomi mia tano na kumi na nne jambo ambalo hakulitarajia kukutana
nalo.
 
“Nimekutana na wasomi wengi
sana leo ambao wamesoma vitu tofauti tofauti na wanauwezo wa kufanya kazi hivyo
ni jukumu langu kuwatafutia sehemu za kupata mafunzo kazini katika makampuni na
mashirika yaliyopo wilaya ya Iringa”alisema Kasesela
 
Nao baadhi ya wasomi waliofika
kwenye zoezi hilo wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
Dr John Pombe Magufuli ikiwakilishwa vizuri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela kwa kuanzisha zoezi hilo.
 
“Kwa zoezi hili limetusaidia
kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu na kutusaidia kupata elimu ya mafunzo kazini na
kusaidia njia rahisi ya kupata ajira kwa kuwa wasomi wanavyoenda kuomba kazi
sehemu mbalimbali” alisema Kasesela
 
Wasomi hao walimpongeza Rais Dr John Pombe Magufuli kwa hatua aliyoichukua kuwatafutia njia mbadala ya kupata ajili kwa wasomi wengi ambao wapo mtaani hawana ajira. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com