METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 20, 2019

JAFO AAGIZA WAUGUZI WALIOHAMISHWA BILA UTARATIBU KUREJESHWA KWENYE VITUO VYAO VYA AWALI

Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Seleman Jafo amemtaka Katibu Mkuu Tamisemi,Joseph Nyamhanga  kuwarejesha katika kituo cha kazi cha Ipogoro Manispaa ya  Iringa watumishi saba ambao walihamishwa hivi karibuni bila kufuata utaratibu.
Waziri Jafo ameyabainisha hayo leo  wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na wilayakote nchini waliokutana Dodoma kujengewa uwezo katika kutekeleza majukumu yao.
Amesema kumekuwa na tabia ya uonevu kwa kushirikiana na wakuu wa vituo hivyo vya afya na kuwahamisha vituo vya kazi jambo ambalo linawafanya wapoteze morali ya kufanya kazi ilihali ni watumishi wanaojituma bila kuchoka.
Aidha,Jafo amemuagiza   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Dk. Zainabu Chaula kufuatilia kama mganga aliyeondolewa kazini kama hakiilitendeka au ni uonevu.
“Kule Iringa Ipogoro watu saba wamesimamamishwa na wewe DMO ni mzuri kwanini  unataka kuharibu ukubwani,Naagiza wale watumishi saba warudishwe na kule nimetuma timu,hatuwezi kulea mambo ya hovyo,” amesema Jafo.
Ameeleza kuwa licha juhudi za serikali bado kuna kazi kubwa ya kuwekeza katika miundombinu ya afya ambapo bado haiko vizuri na kupelekea watumishi kufanya kazi katika mazingira ambayo si rafiki kwao.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Faustine Ndugulile amesema kuna haja ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kusimamia suala la lishe kwani hawafanyi vizuri katika sekta hiyo.
Aidha wamewataka Waganga hao kuwa wachapa kazi na kuacha kulalamika kwani Serikali ipo inafanya jitihada nyingi katika kuboresha maeneo yao ya kazi.
“Lazima mama mjamzito hapaswi kufariki katika kituo cha afya,tafsiri yake kwamba tumeshindwa  hili la vifo vya mama na mtoto ni lazima tuliangalie swala hili kwa upana wake”.amesema Ndungulile.
Naye,Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa,Dk.Paul Chaote akisoma risala,amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba hivyo wakaiomba  serikali kuharakisha mchakato wa bima kwa wote.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com