Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mjs
Deogratius Ndejembi (kulia) akitoa maelekezo kwa mhandisi wa ujenzi wa
bwalo shule ya Sekondari ya Kongwa.
DC Ndejembi akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa madarasa, mabweni katika Shule ya Sekondari Kongwa.
…………………
Na.Alex Sonna,Kongwa
Mkuu wa wilaya ya Kongwa iliyopo
jijini Dodoma Deogratius Ndejembi amesema wahusika wote waliofanya
ubadhilifu wa fedha za ujenzi katika Shule ya Sekondari Kongwa mkoani
Dodoma Watazitapika.
Ndejembi amesema hayo Agosti
9,2019 alipofanya ziara shuleni hapo kwa lengo la kuangalia mwenendo wa
ujenzi wa Shule ya Sekondari Kongwa mradi huo umegharimu zaidi ya
Tsh.Milioni 290 fedha zilizotolewa na Serikali.
Mkuu huyo wa wilaya ametaja
miundombinu inayojengwa katika shule hiyo ni pamoja na mabweni mawili
ambapo kila moja lilitengewa Tsh.Milioni 75 lakini hayatakamilika
kutokana na fedha kuisha,Bwalo lilitengewa milioni 100 lakini nalo pia
halitakamilika kutoka na kubaki mifuko ya saruji 40 pekee .
Hata hivyo, amebainisha kuwa kwa
upande wa Madarasa yatakamilika kwa milioni 36 huku fedha zilizobaki
kwenye akaunti ni milioni 74 pekee ambazo hazitaweza kutosheleza katika
ukamilishaji wa miundombinu yote na zilizobaki nje ya akaunti laki moja
na nusu pekee.
Mhe.Ndejembi amesema sababu
zilizosababisha majengo hayo kutokamilika licha kutengewa fedha nyingi
ni kutokana na kutofuata maelekezo ya Serikali ya kutumia Force akaunti
ambapo walitangaza tenda hali iliyosababisha ununuzi wa vifaa vya ujenzi
kununuliwa kwa bei kubwa tofauti na ilivyo kawaida na ameshangazwa kwa
maeneo mengine hapa nchini yamekamilika.
Hivyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza
TAKUKURU kufuatilia bei ya Manunuzi ya Bidhaa hizo za Ujenzi ,milioni
74 zilizobaki kwenye akaunti zisitume mpaka uchunguzi ukamilike na wale
wote waliohusika katika ubadhilifu huo wanachukuliwa hatua kwa
kumdanganya na kumdharau Rais,Waziri wa TAMISEMI pamoja na yeye.
0 comments:
Post a Comment