Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa
jarida la afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali
zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
jarida la afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali
zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo,upande wa kulia
ni Mhariri Mkuu Msaidizi Jarida la Afya ya Jamii Tanzania Dr.Julius
Massaga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akifungua jarida mara baada ya
kulizindua ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa
hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo,upande wa kulia ni Mhariri Mkuu
Msaidizi Jarida la Afya ya Jamii Tanzania Dr.Julius Massaga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akiwa na baadhi ya viongozi
wakionyesha Jarida la Afya ya jamii mara baada ya kulizindua ambalo
litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo
imefanyika jijini Dodoma leo.
Mhariri Mkuu wa Serikali ambaye pia ni
Mhariri Mkuu wa Jarida hilo Prof.Muhammad Kambi akimueleza jambo Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,mara
baada ya kuzindua Jarida la Afya ya jamii mara ambalo litatumika kutoa
taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma
leo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,akimsikiliza Mganga Mkuu wa Serikali
ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa Jarida hilo Prof.Muhammad Kambi mara baada
ya kuzindua Jarida la Afya ya jamii mara ambalo litatumika kutoa
taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma
leo.
Sehemu ya Muonekano wa Jarida la Afya ya
jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa hafla
hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Sehemu ya wadau wakifatilia uzinduzi wa
Jarida la Afya ya jamii ambalo litatumika kutoa taarifa mbalimbali
zilizochambuliwa hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma leo.
Picha na Alex Mathias
……………………….
Na.Alex Mathias,Dodoma
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto, imezindua jarida la afya ya jamii, ambalo litatumika
kutoa taarifa mbalimbali zilizochambuliwa kisayansi na kuziweka katika
lugha nyepesi ambayo itaeleweka na kila mtu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jarida
hilo, Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu amesema jarida hilo litakuwa na umuhimu mkubwa sana hasa katika
kuleta taarifa kwa jamii zinazotoka katika wizara hilo.
Amewaelekeza wataalamu, wahariri wa
vyombo vya habari na wakurugenzi kutoa taarifa za afya katika jarida
hilo ili taarifa zao ziweze kuwafikia wananchi kwa urahisi kupitia
jarida hilo zitakazo wasaidia wananchi.
“Kuanzishwa kwa jarida hili kutasaidia
sana kwa wananchi kupata taarifa sahihi zilizotoka katika wizara hiyo
na kuzijua kwa undani, pia ni wakati sasa kwa wataalamu, wakurugenzi na
wahariri wa vyombo vya habari kutoa taarifa kupitia jarida hili”
amesema Ummy.
Pia amewaagiza wataalamu wa jarida hilo
kuhakikisha jarida hilo linapatikana kielecronic ili kila mtu aweze
kulipata jarida hilo.
“Ni toe wito kwa wasimamizi wa jarida
hili mhakikishe jarida hili linapatikana kielectrinic mimi pia sio
muumini wa kusoma majarida ila kama likipatikana kielectronic na mimi
nitaweza kupata taarifa hizo” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa
kitengo cha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa yakuambukizwa na
yasiyoya kuambukizwa Dkt Janneth Mghamba , jarida hilo ambalo linatumia
takwimu mbalimbali hapa nchini ambazo zinachambuliwa kisayansi na
kuziweka katika lugha nyepesi.
“Jarida hili litatumia kutoa taarifa
ambazo zimethibitishwa na ambazo zimechambuliwa kisayansi ambazo
zitakuwa zimewekwa katika mfumo rahisi na mwepesi” amesema Mghamba
Amesema jarida hilo litasaidia kujua nini
wizara inafanya na namna wao wanavyoweza kushiriki katika kudhibiti
magonjwa hayo na namna ya kuepukana magonjwa hatarishi.
Amesema jarida hilo ni la kwanza na
litakuwa kama kioo cha wizara ya afya, kioo cha sera kioo cha kutoa
mwelekeo,ufasaha wa sayansi mbalimbali ambazo zinafanyika ndani na nje
ya nchi.
Nae Mhariri msaidizi wa jarida hilo Dkt
Julius Massaga, amesema jarida hilo limetengenezwa kwa takribani mwaka
mmoja kabla ya kuzinduliwa hivi leo litasaidia kutoa taarifa sahihi kwa
jamii ambazo zimethibitishwa na wizara ya afya.
Jarida hilo ambalo limefadhiliwa na CDC
Foundation kutoka Marekani na litakuwa linatoka mara nne kwa mwaka,
lengo ni kutoa taarifa sahihi zinazoandaliwa na wizara ya afya kuwafikia
wananchi kwa urahisi.
Amewataka wadau kuchangamkia fulsa hiyo
kwa ajiri ya kutoa taarifa zao ili ziweze kuwafikia wananchi kiurahisi
na kuzijua taarifa hizo ambazo zitakuwa zimethibitishwa na wizara na
zitakuwa za uhakika.
“Ni wakati wa wadau sasa kujitokeza
kuchangamkia fulsa hii kwa kuleta taarifa ili taarifa zao ziwafikie
wadau wao kwa sababu zitakuwa zinatoka katika sehemu sahihi” amesema
Massaga
0 comments:
Post a Comment