WENYEJI, Misri wametupwa nje ya Fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Afrika Kusini
‘Bafana Bafana’ katika mchezo wa hatua ya 16 Bora usiku wa Jumamosi
Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Shujaa wa Bafana Bafana ni nyota wa Orlando Pirates ya nyumbani, Afrika
Kusini, Thembinkosi Lorch aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 85
akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Lebo Mothiba wa Strasbourg ya
Ufaransa baada ya shambulizi la haraka wakitoka kushambuliwa.
Mshambuliaji wa Liverpool na mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya,
Mohamed Salah alishindwa kuzuia machozi baada ya mchezo huo timu yake,
Misri ikitolewa mapema mno baada ya kushinda mechi zote za Kundi A.
0 comments:
Post a Comment