Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mh
Rais Dr John Pombe Magufuli imejizatiti katika kutekeleza mpango kabambe
wa kuwajengea Ujuzi Vijana kwa lengo la kutatua changamoto ya Ajira ili
kupitia ujuzi watakaoupata katika mafunzo mbalimbali yanayotolewa chini
ya Programu ya kukuza ujuzi inayosimaniwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hayo yamesemwa leo Mirerani,Wilaya ya
Simanjiro-Manyara na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde wakati wa Kongamano la
Wajasiriamali na shindano la kusaka vipaji linaloratibiwa na Mbunge wa
Viti Maalum mkoa wa Manyara Mh Esther Mahawe ambapo Naibu Waziri Mavunde
alitumia fursa hiyo kuelezea mipango mbalimbali ya Serikali katika
kuwajengea ujuzi Vijana wa Kitanzania kupitia program ya kurasimisha
ujuzi,mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba na mafunzo kupitia vyuo vya
Ufundi yote yenye lengo la kumjengea uwezo wa ujuzi kijana wa kitanzania
ili aweze kujiajiri mwenyewe na kuajiri Vijana wengine.
“Ni mpango mkakati wa serikali pia
kuwajengea uwezo Vijana wa Mirerani kupata ujuzi wa kuongeza thamani
katika madini ya Tanzanite ili kuongeza fursa zaidi za Ajira zitokanazo
na sekta hii ya madini”Alisema Mavunde
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mbunge Wa Viti
Maalum Mh Esther Mahawe ameeleza mikakati yake katika kuwakomboa wakina
Mama na Vijana wa Mkoa wa Manyara kwa kuendelea kutoa elimu ya
kujitambua na Ujasiriamali sambamba na kuchangamkia fursa zilizopo
mkoani hapo.
Kongamano hilo lilikwenda sambamba na
shindano fupi la kutafuta vipaji vya wasanii ambao watalelewa na
kufadhiliwa na Ofisi ya Mbunge Esther Mahawe.
0 comments:
Post a Comment