NA
K-VIS BLOG, SABASABA
WANANCHI
wanaofika kwenye banda la Shirika la Umeme nchini (TANESCO), wamesifu hali ya
upatikanaji umeme kwa hivi sasa.
Bw.
Majid Omary ni mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, aliyefika kwenye banda la
TANESCO kwenye viwanja vya Sabasaba kunakofanyika Maonesho ya 43 ya biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam leo Jumapili Julai 7, 2019 alisema
“Kwakweli
mnastahili pongezi, tulikuwa katika shida kubwa ya kupata umeme wa uhakika kwa
muda mrefu, lakini hali kwa sasa imebadilika sana, umeme hausumbui kama
ilivyokuwa hapo awali.” Alisema.
Alisema "Eneo ninakotoka Mbagala Kilungule, tulikabiliwa na tatizo la kupata umeme usiokuwa na nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, pia ulikatika katika, tulisononeka sana lakini tunashukuru Mungu tatizo hilo sasa halipo, hali ya umeme ni nzuri sana." Alisema Bw. Omary
Kama
bado kuna mtu anawalaumu basi ana sababu zake, lakini kwakweli mimi
ninawapongeza sana, nimeona nipite tu hapa kuwapa pongezi, alisema Bw. Omary wakati akizungumza na wahudumu wa TANESCO waliokuwa kwenye kitengo cha huduma
kwa wateja kwenye banda hilo.
Mwingine
aliyepongeza huduma bora za TANESCO ni Bi. Agatha Moses, yeye anatoka Gongolamboto
jijini Dar es Salaam, alisema huduma za umeme zimeimarika sana, kwani katika
eneo anakoishi hawakumbuki ni lini umeme ulikatika.
“Hata
ukikatika inachukua muda mfupi unarejea, sio kama zamani hali ilikuwa tete,
umeme ukikatika ndio basi tena.” Alifafanua.
Aidha
katika banda la TANESCO wananchi wanaalikwa kutembeela kwenye banda hilo
kujipatia huduma mbalimbali kama ambazo zinazotolewa kwenye ofisi za TANESCO.
Leila
Muhaji ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO alisema, wananchi wanaotaka fomu za
maombi ya awali ya kuombea umeme wanaweza kufika kwenye banda hilo na wataalamu
watawapatia fomu bure kabisa.
“Uje
tu na picha ya passport size na
kitambulisho chako utajaza fomu na itachukuliwa hapa hapa Sabasaba na kupelekwa
katika mkoa husika ili maombi yashughulikiwe.” Alifafanua Bi. Leila.
Katika
banda la TANESCO wananchi wanaweza kujionea mashine (mfano) ya kufua umeme wa
maji, ambayo wataalamu wanaonyesha hatua zote kuanzia ufuaji umeme hadi
unapomfikia mteja.
“Pia
unaweza kujinunulia umeme, wapo watu wanokuja kwenye maonesho na inatokea umeme
umeisha nyumbani basi TANESCO tunatoa huduma hiyo kwenye banda na unaweza
mkununua umeme.” Aliongeza Bi. Leila Muhaji.
Mtaalamu kutoka kampuni tanzu ya TANESCO ya uendelezaji jotoardhi Tanzania, (aliyechuchumaa), akiwapatia maeelzo wananchi hawa wakiwemo wanafunzi jinsi jotoardhi linavyoweza kuzalisha umeme, wakati walipotembelea banda la TANESCO Sabasaba Julai 7, 2019.
Mtaalamu wa Mita za umeme, Bi. Matilda Cassian (wakwanza kushoto) akimfafanulia mambo mbalimbali yahusuyo huduma ya kupatiwa mita za umeme kwa mwananchi huyu aliyefika banda la TANESCO Julai 7, 2019.
Afisa Huduma kwa wateja TANESCO, Bw. Khairu Rashid, (kushoto) akimsikilzia mteja aliyefika banda la Shirika hilo Julai 7, 2019. |
Mhandisi Ajuaye Jeggo (wapili kulia) na Mhandisi Esther Mushi, wote kutoka Idara ya usambazaji umeme, wakimsikiliza kwa makini mteja huyu alyetembelea banda la TANESCO Julai 7, 2019.
0 comments:
Post a Comment