Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (wa pili kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa Kampuni ya wazawa ya uchenjuaji dhahabu kwa kutumia mabaki ya mchanga wa dhahabu (MARUDIO) ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd (Hussein Nassoro Amari Kasu (Mb) (wa pili kushoto) katika ukaguzi wa mitambo ya kazi, Jana 6 Machi 2018. Picha zote na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Ukaguzi wa mitambo
Ukaguzi wa mitambo
Naibu waziri wa madini akikagua mitambo mitambo ya Kampuni ya wazawa ya uchenjuaji dhahabu kwa kutumia mabaki ya mchanga wa dhahabu (MARUDIO) ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd, akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita. Jana 6 Machi 2018
Na Mathias Canal, Geita
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameipongeza Kampuni ya wazawa ya
uchenjuaji dhahabu kwa kutumia mabaki ya mchanga wa dhahabu (MARUDIO) ya
Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd inayomilikiwa na Hussein Nassoro Amari Kasu
(Mb) kwa uwekezaji mkubwa iliyoufanya nchini na kuwanufaisha watanzania wengi.
Mhe Biteko ametoa pongezi hizo jana 6 Machi 2018 wakati
akizungumza na uongozi wa kampuni hiyo akiwa katika ziara ya siku moja ya
kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita ambapo pamoja na mambo mengine
anatembelea maeneo ya Wachimbaji wadogo ili kubaini changamoto zinazowakabili
na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema kuwa ni fahari kwa nchi kuwa na wawekezaji wazawa ambao
wanalipa kodi za serikali kwa ufasaha sambamba na kutoa ajira kubwa kwa
watanzania nchini jambo ambalo linaakisi na kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri Wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli.
Kampuni hiyo ambayo huchukua mchanga huo wa madini katika maeneo
mbalimbali nchini zinapofanyika shughuli za kuosha na kuchimba mchanga wa
Madini wa dhahabu imeajiri wafanyakazi wote ambao ni watanzania takribani 60.
Mhe Biteko pia amewataka wafanyakazi wote katika kampuni hiyo
kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa bila kuingiza Mashaka
yoyote kwa mmiliki wa kampuni hiyo.
Sambamba na hayo pia Mhe Biteko ameipongeza kampuni hiyo kwa kuchangia
shughuli Mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati, ujenzi wa
madarasa, Ofisi ya kijiji, ufungaji wa pampu ya maji, pamoja na kutoa mizinga
120 ya nyuki.
Sambamba na hayo kampuni hiyo imeomba kupatiwa ufumbuzi baadhi
ya changamoto ikiwemo kupatiwa maeneo ya kuchimba ili kupata mawe ya kutosha
ili kuwaongezea nguvu katika kuyafikia malengo ya serikali inayoongozwa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kutekeleza kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.
Pia kampuni hiyo imeomba serikali kupatiwa ufumbuzi kwa
kuboresha miundombinu ili kurahisisha kupitisha malighafi kwa kuzifikisha
kiwandani, kusogeza huduma za maji, sambamba na kusogeza huduma za umeme ili
kuongeza ufanisi katika kazi ya uzalishaji.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) ameutaka
uongozi wa kampuni hiyo ya wazawa ya uchenjuaji dhahabu kwa kutumia mabaki
ya mchanga wa dhahabu (MARUDIO) ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings Ltd kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Rais Magufuli anakabiliana na wanyonyaji
wa rasilimali za Taifa na pindi atakapokamilisha juhudi za kuimarisha uchumi,
huduma zote zitapatikana ili kuboresha uwekezaji na maisha ya wananchi kwa
ujumla wake.
MWISHO.
Mimi Nashauri kwa NIA NJEMA tu kwa mwandishi wa makala hii. Kuandika "Ukaguzi wa Mitambo", nadhani SIYO "sahihi, mitambo haikaguliwa na watu wanaoonekana wanapita mbele ya mutambo kwa kasi, halafu wasemekana eti wanakagua. Kukagua mitambo kunaambata na "Utaalamu". Nadhani ni vyema kutumia maneno ya kiswahili kwa usahihi. Mwisho wa kushauri. Naomba msamaha kama nimewakwaza Wasomaji.
ReplyDelete