METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 13, 2019

Shirika la KIVULINI Lakabidhi Vyeti na Kompyuta kwa Viongozi Wachapakazi

Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI limekabidhi vyeti na kompyuta mpakato 11 zenye thamani ya shilingi milioni 13.2 (Tsh. 13,200,000) kwa viongozi mbalimbali wanaoshiriki vema kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Halmashauri ya Wilaya Misungwi.

Akizungumza jana Julai 12, 2019 kwenye zoezi la kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema hatua ni sehemu ya kutambua utendaji kazi bora wa viongozi hao ambao wamesaidia utekelezaji kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.

Aidha Yassin alibainisha kwamba kupitia juhudi za viongozi hao, kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi pia kimeongezeka katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019 katika shule mbili za mfano ambazo ni Shule ya Wasichana Bwiru pamoja na Misungwi Sekondari.

Naye mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyekuwa mgeni rasmi, alikemea baadhi ya wanaume wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike na kutoa rai kwa shirika la KIVULINI kuendelea kusaidia utoaji elimu hadi ngazi ya jamii ili kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Viongozi waliopata vyeti na kompyuta mpakato (Laptops) ni mbunge jimbo la Ilemela, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Afisa Elimu Sekondari Ilemela, Mkuu wa Shule ya Wasichana Bwiru.

Wengine ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Afisa Elimu Sekondari Misungwi, Afisa Maendeleo ya Jamii Misungwi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Misungwi pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Chato.
 Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza baada ya zoezi la kukabidhi kompyuta mpakazo kwa viongozi mbalimbali Ilemela na Misungwi.
 Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi cheti kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Afisa Elimu Sekondari wilayani Misungwi, Mwl. Diana Kuboja (kushoto).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Misungwi.
Jedwali likionesha kiwango cha ufaulu kilivyopanda katika Shule ya Wasichana Bwiru wilayani Ilemela pamoja na Misungwi Sekondari wilayani Misungwi kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu 2019.
 Wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
 Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com