Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(kushoto) akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Busega, Itilima na
Bariadi katika majumuisho ya Ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
mkoa katika Hospitali za Wilaya hizo, iliyofanyika Julai 04,2019. .
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson
Kilangi(kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kukagua ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya ya Itilima, Julai 04, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(mwenye koti jeusi) na viongozi wengine wakitoa katika moja ya
majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bariadi wakati wa ziara maalum ya
kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika Julai 04,2019
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(mwenye shati la kitenge mbele) na viongozi wengine wakitoa katika
moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega wakati wa ziara maalum
ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika julai 04, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(mwenye shati la kitenge mbele) na viongozi wengine wakitoa katika
moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega wakati wa ziara maalum
ya kukagua ujenzi wa hospitali hiyo iliyofanyika Julai 04, 2019
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakikagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bariadi Julai 3, 2019.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Busega yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bariadi yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi
………………………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka
amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa wahandisi wa ujenzi
kuwatambua na kuwajengea uwezo mafundi wote wanaotoka kwenye jamii
wanaofanya kazi za serikali kwa kutumia mfumo wa ujenzi usiotumia
wakandarasi (Force Account) hususani waliofanya kazi nzuri kwenye ujenzi
wa hospitali za wilaya ya Mkoa wa Simiyu.
Mtaka ameyasema hayo mara baada ya
kufanya ziara katika hospitali za wilaya ya Itilima, Bariadi na Busega
zinazoendelea kujengwa lengo ni kujua hatua ziizofikiwa katika ujenzi,
ambapo amesema mafundi hao wakitambuliwa na kujengewa uwezo utendaji
wao utaimarishwa na kazi watakazofanya zitafanywa katika ubora.
“Ni lazima kama Mkoa tuwe na mfumo wa
kuwatambua mafundi wote waliofanya kazi ya kujenga hospitali zetu zote
tatu na tuanze kuwajengea uwezo,ili miradi yetu ya Serikali
tunayoendelea kuifanya tusiwe na watu wapya sana na kama tukipata wapya
watakuwa wanafanya kazi chini ya uangalizi wa watu wenye uwezo mzuri
zaidi” Mtaka
Mbali na hayo amezipongeza wilaya hizo
kwa mfumo walioutumia wa kununua vifaa kiwandani moja kwa moja kwani
umesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zimefanikisha ujenzi kufikia katika
hatua nzuri, huku akizisisitiza wilaya hizo kuwashirikisha Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) kwenye ununuzi wa vifaa vya umeme ili kupunguza
gharama zisizo za lazima.
Kwa upande wao Wakurugenzi wa Halmashauri
za wilaya SACF James John (Bariadi) Elizabeth Gumbo (Itilima) wamesema
kuwa miongoni mwa changamoto zilizopelekea kutokamilisha kwa miradi
hiyo ambayo ilitakiwa kukamilika Juni 30 , 2019 ni fedha kutotosheleza
na kusisitiza kuwa ikiwa watapokea fedha mapema watakamilisha majengo
yote.
“Tulipokea bilioni 1.5 tumebakiwa na
shilingi milioni 75 kwa ajili ya kulipa mafundi tulioingia nao mkataba,
ili tuweze kukamilisha hatua zilizosalia katika ujenzi wa majengo saba
ya awali tunahitaji shilingi milioni 370” alisema James John mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
“Tulipokea shilingi bilioni 1.5
tumebakiwa na shilingi milioni ambazoo zimetengwa kwa ajili ya malipo ya
mafundi, tukiongezewa shilingi milioni 360 tutamaliza majengo kwa hatua
zilizobaki” alisema Elizabeth Gumbo mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya
ya Itilima.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano
Mwera amebainisha kuwa kwa hatua walioyofikia fedha zinatosha
kukamilisha mradi na kwamba changamoto iliyopelekea wasiweze kukamilisha
kwa wakati ni ucheleweshwaji wa mfumo na kwamba ikifanyiwa kazi mradi
utakamilika kwa wakati.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini amesisitiza Halmashauri za Wilaya ya Bariadi, Busega na
Itilima kumalizia ujenzi wa Hospitali za wilaya kwa wakati ambapo pia
alitoa rai ya kuhakikisha barabara zinatengenezwa, miti na bustani za
maua zinapandwa katika maeneo hayo ambayo hospitali hizo zinajengwa.
Katika ujenzi wa hospitali za wilaya ya
Bariadi, Itilima na Busega ambao ni wa awamu ya kwanza kuna jumla ya
majengo takribani ishirini na moja yanapaswa kujengwa (21) ikiwa ni
majengo saba kwa kila Hospitali (kwa awamu ya kwanza) ambayo yapo katika
hatua mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment