Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA
Mhandisi Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akiwaongoza wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu kukagua ujenzi wa Jengo la
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Julai 04, 2019.
Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA
Mhandisi Likimaitare Naunga akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera
akizungumza majumuisho ya ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Julai 04, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini akizungumza katika majumuisho ya ziara ya Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka( wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakikagua ujenzi wa Jengo la
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega, Julai 04, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka( wa sita kushoto) katika picha ya pamoja na viongzoi mabalimbali
wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua ujenzi
wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega unaoendelea wilayani
Busega, Julai 04, 2019.
Sehemu ya nyuma ya Jengo la Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Busaga ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka
huu na wananchi kuanza kupata huduma.
……………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka imeridhishwa na
kasi ya Ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega na
majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, chini ya Mkandarasi
Wakala wa Majengo nchini (TBA ).
Hayo yamebainishwa na kamati hiyo ,mara
baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Busega
ambapo ujenzi umeanza mwezi Aprili mwaka huu na unatarajia kukamilika
ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amesema miradi yote inayotekelezwa na TBA Simiyu imekuwa
ikitekelezwa kwa wakati na wakati mwingine imekuwa ikitekelezwa na
kukamilika kabla ya muda uliopangwa katika mkataba, huku akiishukuru
serikali kwa kutenga fedha za ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya
Busega ambayo itatua changamoto za wananchi za upatikanaji wa huduma
kwa karibu .
“Tumepata Meneja mzuri wa TBA ambaye
anatekeleza miradi yake kwa wakati, miradi yote tuliyompa imetekelezwa
mbele ya muda uliowekwa kwenye mkataba; kwa mradi huu umeenda kwa kasi
ambayo inaendana na uhitaji wa wananchi wa Busega waliokuwa wanahitaji
mahali pa kupata huduma” alisema Mtaka.
Mkuu wa wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera
amesema utendaji wa kazi kwa sasa ni mgumu kutokana na ufinyu wa jengo
wanalolitumia kama ofisi, hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutawasaidia
kufanya kazi kwa ufanisi.
“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutupa fedha za
ujenzi wa jengo hili, litakapo kamilika litatuwezesha kufanya kazi kwa
ufanisi kwa sababu ofisi tunayoitumia sasa hivi ni finyu sana na
watendaji wametawanyika sana hivyo inatuwia vigumu kiutendaji”alisema
Mwera.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini amesema kazi zote zinazofanywa na Wakala wa majengo
nchini TBA Mkoa wa Simiyu zimekuwa zikifanywa kwa viwango na
zinakamilika kwa wakati, huku akiahidi kulipa fedha zilizobakia kwa
wakati.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa
Majengo nchini TBA Mhandisi Likimaitare Naunga amesema mkataba wa ujenzi
wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega ni miezi mitano na wanatarajia
kukamilisha ujenzi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Kukamilika kwa ujenzi awamu ya kwanza ya jengo hilo utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia saba nukta saba.
0 comments:
Post a Comment