METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 15, 2021

"Tumekusudia kuendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wa Viuatilifu wasiofuata Taratibu na Sheria"Dkt. Efrem Njau


Pichani: Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) Dkt. Efrem Njau akihutubia washirikiwa wa mafunzo ya 54 ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, sheria na kanuni za udhibiti wa viuatilifu,Picha zote na Innocent Natai 

Kaimu Mkukuu wa Idara ya Utafiti-TPRI Prof Eliningaya Kweka(Kulia)akisikiliza risala ya wahitimu wa mafunzo ya 54 ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, sheria na kanuni za udhibiti wa viuatilifu



Pichani: Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) Dkt. Efrem Njau akitoa zawadi kwa mmoja kati ya wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo

Picha ya Pamoja kati ya Menejimenti ya Taasisi ya TPRI na wahitimu wa m mafunzo ya 54 ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, sheria na kanuni za udhibiti wa viuatilifu


Na Innocent Natai

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) Dkt. Efrem Njau amewataka wafanyabiashara wa viuatilifu wanaofanya biashara bila kufuata taratibu na sheria kuacha mara moja kwani inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo bora

 Ameyasema hayo hivi leo Makao makuu ya Taasisi hiyo Arusha wakati wa akiahirisha mafunzo ya 54 ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, sheria na kanuni za udhibiti wa viuatilifu yaliyo tolewa kwa Wakulima, Wanafunzi, Watumishi wa Makampuni ya viuatilifu na Maafisa Ugani yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kuweza kufanya biashara za viautilifu kwa usahihi na kwenda kuwasaidia wakulima kutumia viuatilifu kwa usalama zaidi  

Dkt. Njau amesema kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara za viuatilifu wanaofanya biashara hiyo bila kupata mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu kitendo kinachopelekea kuwauzia wakulima viuatilifua ambavyo havikidhi vigezo na pia kushindwa kuwapa ushauri wakulima wa kiuatilifu gani kinatumika kwa mazao yake na kwa wakati gani 

“kwa kujifunza kozi hii tunaimani mtakuwa hamuuzi wala kusambaza viuatilifu ambavyo havija sajiliwa na Taasisi ya TPRI mjue kwamba ukikutwa unauza au unasambaza viuatilifu ambavyo havijafanyiwa utafiti na kuthibitishwa na TPRI ni kosa la kisheria na tutakuchukulia hatua kali” Dkt. Efrem Njau 

Aidha amewataka kuwa mabalozi huko kwenye mikoa waliyotoa kwa kutumia vizuri elimu waliyoipata na endapo wataona mfanyabiashara anafanya biashara kinyume na taratibu na sheria watoe taarifa mara moja ili mfanyabiashara huyo achukuliwe hatua kunusuru wakulima

Dkt. Njau amesema wa hitimu wa mafunzo hayo watakuwa na uwezo sasa wa uuzaji, ufukizaji, usambazaji na uzalishaji  kwa kufuata na Sheria, Kanuni na taratibu zilizoko hapa nchini, Kujua  na kutambua viuatilifu vilivyosajiliwa na TPRI, Kuweza  kujua na kutambua aina mbalimbali za vinyunyizi/Vipulizi na stadi sahihi za kutumia vinyunyizi na vinyunyizo wakati wa kunyunyizia au kupulizia viuatilifu kwenye mazao, Kujua  aina mbalimbali ya Viuatilifu, kutambua athari za viuatilifu kwa afya ya binadamu, wanyama na jinsi viuatilifu vinavyoweza kusababisha uchafuzi wa mazingira, Kujua namna ya kusajili biashara ya viuatilifu kwa njia rafiki na rahisi popote uwapo kwa kutumia teknolojia ya mtandao ambayo ni Agriculural Trade Management Information system (ATMIS).

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake bi Salima Mngonja amekiri kutokuwa na ulelewa mpana wa ufanyaji wa biashara za viuatilifu na viuatilifu kwa ujumla kabla ya kupatiwa mafunzo hayo, hivyo basi baada ya kupatiwa elimu hiyo watakwenda kufanya biashara hiyo kwa ustadi mkubwa huku wakifuata sheria, kanuni na taratibu zilizo wekwa

Aidha ameiomba serikali kuiwezesha taasisi ya TPRI ili iweze kutoa zaidi mafunzo hayo kwa wakulima,Watumishi wa Makampuni ya viuatilifu na Maafisa Ugani nchi nzima ili kuwasaidia wakulima kujikwamua kwa kupata pembejeo bora na kwa bei nafuu.


Mafunzo hayo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, sheria na kanuni za udhibiti wa viuatilifu hutolewa kwa Wakulima, Wanafunzi, Watumishi wa Makampuni ya viuatilifu na Maafisa Ugani mara mbili kwa mwaka Makao Makuu ya Taasisi ya TPRI Arusha Ngaramtoni na mikoani 



 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com