Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
Maafisa wa Kampuni ya uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya Kilimo ya Seed Co.
wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda
mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa
wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo
Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa
Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wa ziara yake aliyoifanya
leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa
maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika
Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ziara yake aliyoifanya leo Jumamosi (Julai
6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya washiriki wa maonesho ya 43 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mmoja wa Maafisa
wa Idara ya Sera na Machapisho wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa ziara
aliyoifanya leo Jumamosi (Julai 6, 2019) kutembelea mabanda mbalimbali ya
washiriki wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
****************
Na Mwandishi Wetu
MAELEZO
DAR ES SALAAM
6. JULAI, 2019
RAIS
Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amezipongeza Wizara ya
Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TANTRADE) kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya 43 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius
Nyerere.
Akizungumza
leo Jumamosi (Julai 6, 2019) mara baada ya kutembelea na kukagua
mabanda mbalimbali ya washiriki wa Maonesho hayo, Rais Mstaafu Kikwete
alisema hizo ni dalili njema kwa maonesho hayo kwa kuwa yamekuwa bora
zaidi ya maonesho yaliyofanyika mwaka jana.
Aidha
aliongeza kuwa maonesho ya mwaka huu, yameonesha dhamira ya dhati ya
Serikali katika kujenga uchumi wake kupitia viwanda, kwa kuwa katika
maonesho ya mwaka huu malighafi nyingi za kilimo zimepewa kipaumbele na
wazalishaji wa bidhaa mbalimbali.
“Maonesho
ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi, kwani tumeshuhudia malighafi nyingi
za kilimo zikipewa kipaumbele na hii imekuwa ni dalili njema na point
(alama) tunayotakiwa kuifikia kwa sasa” alisema Kikwete.
Awali
akitembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rais Mstafu Kikwete
alilitaka jeshi hilo kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa bora
zitakazoweza kutumika nje ya Tanzania hususani bidhaa za ngozi ikiwemo
viatu vinavyozalishwa na Jeshi hilo.
0 comments:
Post a Comment