Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako ameagiza Mwongozo wa Kutambua na Kuendeleza
Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia uhuishwe ili kuwa na wigo mpana wa
kutambua wabunifu kuwezesha na kuwaendeleza.
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo
jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Ubunifu cha kampuni ya
Jematech ambapo amesema miongozo iliyopo na inayoandaliwa iwe ya rahisi
na shirikishi.
Aidha amesema muongozo uliopo wa kutambua
wabunifu uhuishwe ili kutoa nafasi pana zaidi kwa bunifu mbalimbali
kutambulika kwa taratibu rahisi na rafiki kwa wadau badala ya kuwa na
taratibu ngumu za kuwakatisha tamaa na kushindwa kuendelea na bunifu
zao.
“Tumepewa dhamana ya kusimamia masuala ya
sayansi, teknolojia na ubunifu sisi tusiwe kikwazo kwa watu ambao
wanamawazo mazuri bali tuwe wawezeshaji ili tuwawezeshe ndoto na bunifu
zao kunufaisha watanzania” amesema Ndalichako.
Akizungumzia kituo hicho Prof. Ndalichako
amesema amefarijika kuona kampuni ya Jematech imeamua kuwekeza na
kuendeleza ubunifu nchini kwa kuanzisha kituo cha teknolojia jijini
Mwanza, kwani ni cha kisasa kizuri chenye miundombinu na vifaa vya
kisasa vya kiteknolojia.
Amesema amefarijika kuona kituo cha Jema
kinatoa fursa kwa vijana wa kitanzania wenye ubunifu kutumia miundo
mbinu ya kituo hicho na pia kupata nafasi ya kujifunza na kuendeleza
mbunifu zao huku haki miliki ya bunifu kubaki kwa vijana hao.
“Kwa hiyo watatoa fursa kwa vijana
wanaojihusisha na ubunifu wa kijiditali kuweza kujiendeleza na kutatua
changamoto mbalimbali katika jamii yetu na nimefarijika sana kuona
tayari wanatoa fursa kwa wanafunzi waliopo vyuo vikuu vyetu kutumia
kituo chao bure na kuwa watatoa ushauri na kuwasaidia kiendeleza bunifu
zao, huu ndio utekelezaji wa dhani shirikishi na srkta binafsi amesema
Waziri Ndalichako”
Aidha, Profesa Ndalichako ameitaka Tume
ya Sayansi na Teknolojia kubadilika kwa kutambua kuwa ubunifu ni mtu
kufanya kitu ambacho ni zaidi ya kile unachofanya ama kukijua na
kutambua kuwa sekta binafsi ina mchango katika kuendeleza teknolojia na
ubunifu hivyo washirikiane nao kwa karibu.
Ndalichako amepongeza Vijana waanzilishi
wa Kampuni hiyo hapa nchini akiwemo Mkurugenzi Mtendaji na Injinia Mkuu
ambao ni zao la shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma walipata nafasi ya
kwenda kusoma na kuishi nje ya nchi lakini wameamua kurudi na kutumia
ujuzi walioupata kuendeleza nchi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella
amesema ajira kubwa sasa iko katika eneo la teknolojia kwenye TEHAMA
ambapo amesisitiza ndiko duniani inakokwenda.
Mongella amesema kama Taifa kuna kazi
kubwa ya kujenga vituo vya ubunifu kwani mpaka sasa haijawekezwa vya
kutosha. Amemuomba Waziri Ndalichako kusimamia hilo ili kutoa fursa kwa
vijana wengi kote nchini wenye ubunifu mkubwa ila hawajapata fursa ya
kuziendeleza.
Awali Mkurugenzzi Mkuu wa Jematech
Jumanne Mokili alimweleza Waziri kuwa Kituo hicho kinalenga kutumia
mawazo ya pekee, fursa raslimaliwatu na vitu vinavyopatikana nchini
kutatua changamoto katika jamii na kwa kutumia teknolojia na ubunifu.
Amesema lengo la Jema ni kuiona Tanzania
kuwa kampuni kubwa yenye kuleta ushindani katika makampuni makubwa
Duniani ya teknolojia na ili kutimiza hilo unahitajika uwekezaji
madhubuti na dhati wa rasilimaliwatu, hivyo imewaleta pamoja wahandisi
wake waliopo Tanzania, Japan na Marekani ili kubadilishana ujuzi na
kubuni mifumo itakayotatua changamoto za kimfu
mo katika maeneo ya kilimo, afya ,elimu na biashara chini .
0 comments:
Post a Comment