Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akieleza umuhimu wa Taasisi za dini
katika kujenga ustawi wa Taifa, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akieleza umuhimu wa Taasisi za dini
katika kujenga ustawi wa Taifa, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam,
Baadhi ya washiriki wa Kongamano
la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe
25 Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) (katikati), akicheza moja ya nyimbo
za kwaya, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifanyiwa maombi maalumu na
waratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam,.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimkabidhi sadaka Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Mchungaji Deborah Malassy, wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Mchungaji Deborah Malassy, akihubiri wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam. Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Baadhi ya washiriki na waalikwa katika Kongamano
la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe
25 Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Askofu Dkt. Godfrey Malassy, akihubiri wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam. Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la
Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe 25
Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui
ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………………
Na. OWM, DAR ES SALAAM.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama (Mb), ameeleza kuwa serikali inatambua juhudi za taasisi za dini
hapa nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu, hivyo
itaendelea kushirikiana na taasisi hizo katika kuunga juhudi za serkali
za kujenga amani, umoja, upendo na mshikamano na hatimaye kuleta
ustawi wa Taifa.
“Napenda kuwahakikishia ushirikiano wa
serikali katika kutekeleza majukumu yenu ya kiroho na ya huduma za
kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya watanzania. Pale mtakapoona mchango
wa serikali unahitajika msisite kuwasiliana nasi. Na iwapo mtaona kuna
upungufu wowote semeni kwa viongozi wa wilaya, mkoa na wa kitaifa. Sisi
ni wasikivu. Tuite tutawaitikia, tutatenda kwa lile ambalo lipo ndani ya
uwezo wetu” amesisitiza Mhe. Mhagama.
Akiongea kwa niaba ya Mheshimiwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, katika Kongamano la maombi ya wanawake waombolezao, jijini Dar
es salaam, tarehe 25 Julai, 2019, Mhe. Waziri Mhagama amefafanua kuwa
waratibu wa Kongamano hilo wanapongezwa na viongozi wote serikalini,
akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli, kwakuwa linachagiza maendeleo katika Taifa hili na ustawi wa
watu wake.
“Viongozi wetu kwa pamoja ni shupavu,
wanaoaminiwa na kutumainiwa na wananchi hasa wanyonge. Viongozi
wanachukia na kupinga rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa
vitendo na Rais anayejipambanua kwa kufanya maamuzi magumu ya kulinda
rasilimali za Taifa. Lakini haya yote yamewezekana kwa kuwa
wamejikabidhi katika mikono ya Mungu na nyie mmekuwa mkiwaombea” amesema
Mhe. Mhagama.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mhagama
amewataka Wanawawake waombolezao waendelee kumuombea Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ambazo
anaendelea kuzifanya tangu aliposhika hatamu ya uongozi, kwa kuthubutu
kutenda na kuiletea nchi mafanikio makubwa.
“Kwa uchache kazi kubwa ambazo
amezitekeleza Mhe. Rais, ni pamoja na kutoa elimu ya msingi bila malipo
ambapo ameweza kuwagusa hata walewasiojiweza, kuongeza bajeti ya dawa,
vifaa tiba na vitendanishi na kujenga Hospitali na Vituo vya Afya vingi
ili watanzania wengi wapate huduma za Afya kwa karibu. Pia umeme kwa
sasa umesambazwa vijijini kupitia mradi wa REA na sasa mradi mkubwa wa
uzalishaji umeme wa Maji (Rufiji) umeanzishwa” amesisitiza Mhagama.
Awali wakiongea katika Kongamano hilo,
waratibu wa Kongamano hilo, Mchungaji Deborah Malassy na Askofu Dkt.
Godfrey Malassy wamebainisha kuwa wameamua kuendesha Kongamano hilo kwa
kuwa wanatambua kuwa viongozi wa dini kama walivyo wa serikali wanao
wajibu maalamu wa kulilea Taifa. Aidha wameongeza kuwa ushirikiano
ukiwa imara watafanikiwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano uliopo
hapa nchini.
“Tutaendelea kutekeleza wajibu pekee wa
kujenga uhai wa Taifa letu na watu wake. Tunampongeza Mhe.Rais wetu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uongozi
wake bora uliokidhi kiu na kilio cha watanzania kwani tumeona jitihada
anazofanya pamoja na kutiwa moyo na kazi zake anazozifanya na viongozi
wote wa serikali ya awamu ya tano. Kwa hamasa hii tunapata nguvu ya
kuendelea na wajibu huu mkubwa tuliopewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea
kuliombea Taifa letu” amesema, Mchungaji Deborah.
Kongamano hilo la kumi la Kihistoria hapa
nchini liliohusisha Wanawake Waombolezao Kitaifa kutoka mikoa yote
Tanzania na Zanzibar, pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali,
limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Kongamano hilo ni sehemu ya Maombi ya kila mwisho wa mwaka wa tarehe 31
Disemba ya kuliombea Taifa hili yajulikanayo kama MKESHA MKUBWA KITAIFA
DUA MAALUM, ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya wazi katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment