METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, July 2, 2019

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU ATEMBELEA BANDA LA WAKALA WA VIPIMO KATIKA MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akiangalia vipimo vinavyotumiwa na Wakala wa Vipimo alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akioneshwa kigezi (standard) kinachotumia kupimia mizani ya madini na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akipata maelezo juu ya majukumu ya WMA kutoka kwa  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akioneshwa  vifaa vya kitaalam vinavyotumiwa na WMA katika kutimiza majukumu yake na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
……………….

Jumuiya ya wafanyabiashara watakiwa kutoendelea kutegemea kuuza nje bidhaa ghafi bali watumie viwanda vya nyumbani na bidhaa hizo ziongezwe thamani kwa kusindikwa na kufungashwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Ameyasema hay oleo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari katika sherehe hizo Mh. Samia amesema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara ina jukumu la kuwandaa wanachama wake kuwa na ufahamu wa kutosha, kuwa na uthubutu na kutayarisha miradi na kuwa tayari kupambana katika medani ya biashara.

“Ili Tanzania iweze kukidhi mahitaji ya fursa za masoko ya biashara zao, tunahitaji kufanya kazi kwa bidii kwa kuzalisha bidhaa zenye ushindani”. Amesema Mh. Samia.

Aidha, Mh. Samia amesema kuwa ili ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ushike kasi ya kutosha, hakuna budi kwa sekta kama kama vile kilimo, mifugo,Uvuvi na madini kutoa malighafi za kutosheleza viwanda hivyo.

“Wakati tunahimiza ujenzi wa Uchumi wa Viwanda msukumo tunauweka pia kwenye sekta zinazozalisha malighafi.Sekta ya kilimo ikijipanga vema, viwanda vitapata malighafi hivyo hivyo kwa sekta ya mifugo, uvuvi, madini na sekta nyingine”. Ameongeza Mh. Samia.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com