Waziri wa Madini Doto Biteko katikati
kulia na Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila katikati kushoto wakiwa
wanasikiliza jambo huku Afisa Madini Mkazi mkoa wa Mara Nyaisaara Mgaya
wakati wa kikao cha usuluhishi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa
madini ya dhahabu eneo la Ikungi mkoani Mara na Kampuni ya PolyGold (T)
Ltd.
Sosy Mgonya miongoni wa wachimbaji wadogo akijibu swali aliloulizwa na Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Madini Doto Biteko katikati
kulia, Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila katikati kushoto na Mtendaji
Mkuu wa Tume ya Madini Prof. Shukrani Manya wakiwa kwenye kikao cha
usuluhishi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu
eneo la Ikungi mkoani Mara na Kampuni ya PolyGold (T) Ltd hawapo
pichani.
…………………………..
Na Issa Mtuwa -WM – Dodoma
Uwe mzawa, uwe mwekezaji wa nje kwangu
haki yako utaipata. Ni kauli ya Waziri wa Madini Doto Biteko wakati
akisuluhisha mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu
eneo la Ikungi mkoani Mara na mwekezaji wa kampuni ya PolyGold (T) Ltd.
Ametoa kauli hiyo leo Julai 2, 2019
ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma baada ya kukutana na pande hizo
mbili ambazo awali zilikubaliana na kusainiana mkataba wa kuchimba
madini kwa ushirika. Pande hizo zilishindana kabla ya kuanza kwa shuguli
za uchimbaji kiasi cha kuwa na mgogoro mkubwa uliopelekea kufikishana
kwa Waziri wa Madini ili kupata suluhu ya mgogoro wao ambao teyari
umetatuliwa na Waziri Biteko.
Akitumia staili ya ushirikishi wa
kusikiliza kila upande, Biteko alitoa fursa ya kila upande kuongea na
kubaini changamoto kadhaa. Baada ya kuwasikiliza, Biteko alifikia
maamuzi ya kuwatoa nje wawakilishi wa Kampuni ya PolyGold (T) Ltd nje ya
ukumbi wa kikao ili azungumze na wachimbaji wadogo baada ya kugundua
changamoto kwa upande wao.
Hali aikuwa shwari kwa muda baada ya
Biteko kucharuka baada ya kubaini uwepo wa ujanja ujunja kwa upande wa
wachimbaji wadogo na kuwataka waache ujanja ujanja na kusikiliza maneno
ya watu walio nje na makubaliano na mshirika wao na kuwaambia waache
tamaa badala yake waheshimu makubaliano waliyofikia kwa hiyari yao bila
uwepo wa wizara.
Amesema yapo malalamiko ya wawekezaji
katika maeneo mbalimbali ya uwekezaji hivyo hataki kuruhusu ujanja
ujanja huo utokee kwenye wizara anayo iongoza. Ameongeza kuwa hata kama
wao ni kutoka nje wanayo haki ya msingi kupewe haki yao pale
inapoonekana kukiukwa au kuonewa kwani shuguli zao ni halali na
wanafuata sheria.
“Ndugu zangu niwaambie ukweli, huyu mmoja
mnae muona (Mwekezaji) ana haki kama nyinyi, akionewa huyo mjue anawatu
yuma yake, ana ubalozi hapa kwa hiyo siko teyari kuchafua jina la
serikali na wizara ninayo iongoza kwa kukiuka haki ya upande fulani. Uwe
mzawa uwe mwekezaji wa nje kwangu haki yako utaipata, kwa hiyo kaeni na
mkubaliane na mwekezaji wenu, mimi na wezangu tunatoka tunawacha
nikirudi tupate majibu msimamo wangu nimewapa”. alisema Biteko huku
akiwa amekasirika.
Mara baada ya maelekezo hayo wachimbaji
wadogo wakiongozwa na Edwin Mchihiyo na Sosy Mgonya ambae leseni yake
imenusurika kufutwa na waziri walikaa pamoja na mwekezaji wao kampuni ya
PolyGold (T) Ltd iliyo wakilishwa na Sergey Sagsyan na Benny Haule na
kuzungumza kuhusu mvutano juu ya mgogoro wao na kufikia muafaka
uliopelekea kuondoa mgogoro uliokuwepo.
Akiongea kwa niaba ya wenzake kiongozi wa
wachimbaji hao wadogo Edwin Mchihiyo amemshukuru Waziri kwa kusimamia
kutatua mgogoro wao ambao umefikia tamati na kuahidi wanakwenda
kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yanaleta sinto fahau baina yao.
Katika kikao hicho Waziri aliambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mtendaji Mkuu wa
Tume ya Madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu Issa Nchasi na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge wote
kutoka wizara ya madini na viongozi wengine wa Wizara na Tume ya Madini.
0 comments:
Post a Comment