





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 07,2019
amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaojadili masuala
mbalimbali kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika (AFRICAN CONTINENRAL
FREE TRADE AREA – AFCFTA) Mkutano huo unaofanyika mjini Niamey Nchini
Niger umefunguliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU Rais Abdel
Fattah el Sisi wa Egypt. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
0 comments:
Post a Comment