Martin Massawe wa NMB akimlamba chenga
Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) katika mechi ya soka ya Bonanza la
Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22,
2019. Bunge ilishinda 5-3.
Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) akizuia
mpira huku akizongwa na Martin Massawe wa Bunge katika mechi ya soka ya
Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri
jijini Dodoma Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5-3.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi
Kikombe nahodha wa timu ya soka ya Bunge, Cosato Chumi baada ya timu
yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya timu ya NMB katika mchi ya
Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma, Juni 22, 2019. Kushoto ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Mwansasu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) wakimtazama nahodha
wa timu ya Soka ya Bunge, Cosato Chumi aliponyanyua kikombe cha ushindi
wa mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa
Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5 – 3. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni
muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa
inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 22,
2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB
lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha
afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha
mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.
Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya
NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima
umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.
“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu
kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa
huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”
Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo
ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu
ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete
timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli
25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda
baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.
Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.
0 comments:
Post a Comment