Naibu waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea mgodi wa wachimbaji wadogo Kitunda uliopo Wilayani Sikonge, Jana 25 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika mgodi wa wachimbaji wadogo Kitunda uliopo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora, Jana 25 Februari 2018.
Naibu waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na Sospita Haruna Ibrahimu ambaye anafanya kazi za uchimbaji katika mgodi wa wachimbaji wadogo Kitunda uliopo Wilayani Sikonge, Jana 25 Februari 2018. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe Peres Boniface Magiri
Na Mathias Canal, Tabora
Baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika mikoa ya Rukwa na
Katavi Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewasili
Mkoani Tabora ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea na kukagua utendaji
kazi katika mgodi wa wachimbaji wadogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
Jana 25 Februari 2018 Mhe Biteko alitembelea mgodi wa wachimbaji
wadogo Kitunda uliopo Wilayani Sikonge ambapo alizungumza na wafanyakazi katika
mgodi huo ambao una uwezo wa kuajiri wafanyakazi kati ya 5000 mpaka 10,000.
Mhe Biteko aliwaeleza wachimbaji hao kuwa serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John
Pombe Magufuli imekusudia kuondoa manyanyaso kwa wananchi.
Aidha, alielezea mikakati ya serikali katika sekta ya Madini
hususani umuhimu wa ulipaji kodi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment