Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani,akizungumza na watumishi wa Tanesco na wa REA kabla ya kuanza kwa kikao
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu,akitoa rai kwa watumishi wa Tanesco na REA katika kikao cha
kujadili mambo mbalimbali ya umeme kilichofanyika jijini Dodoma.
katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dk. Hamis
Mwinyimvua,akitoa taarifa kwa Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleamni
kabla ya kufungua kikao cha watumishi wa Tanesco na REA kilichofanyika
leo jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kaleamni,akizungumza wakati wa kufungua kikao cha watumishi wa Tanesco
na REA kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya baadhi ya watumishi wa Tanesco
na REA wakifatilia kwa makini kikao cha Waziri wa Nishati Dkt.Medard
Kaleamni kilichokuwa na lengo la kuwakutanisha na kutatua changamoto
mbalimbali za umeme kilichofanyika leo jijini Dodoma.
……………………..
Na.Alex Mathias,Dodoma.
Serikali imesema itaanza kuwatambua
wazalishaji wadogo wa umeme na kuwasimamia hata kama wanazalisha umeme
kwa kiasi kidogo sana.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodma Waziri wa
Nishati Dkt Medard Kalemani ,wakati wa kikao baina yake na watumishi wa
Tanesco na wa mradi wa umeme vijijini REA.
Dkt.Kalemani amesema kuwa ni wajibu wa
Tanesco na REA kuwatambua wazalishaji wadogo wa umeme ifike mahali
ufanyike utafiti unaoweza kusaidia kuongeza umeme, na wale wenye
leseni za EWURA.
“Tuhakikishe kuwa tuwatambue tuwasimamie
na tuwaingize, hivyo REA na Tanesco wawasimamie wana mchango mkubwa
sana katika hili” amesisitiza Dkt.Kalemani
Aidha amesema kuwa watendaji hao wameitwa
ili kutafakari walichokifanya 2018/2019 na kujipanga upya kutekeleza
majukumu yao katika mwaka wa fedha unaoanza julai ili kuhakikisha huduma
zinakuwa imara muda wote.
Dkt.Kalemani amesema kuwa lengo lengo
letu ni kuhakikisha kuwa tunakwenda kutekeleza majukumu yetu ili
kutimiza azima ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda bila sekta hii
hatuwezi kufikia malengo ya serikali.
Hata hivyo amefafanua baadhi ya
changamoto zilizopo katika gridi ya taifa, tumeondokana na mashine kule
Ngara bado kuna changamoto watu wanasema bora tubaki na mafuta yetu,
tumepeleka gridi kwa lengo la kutatua kero lakini inazidi, Liwale, Geita
changamoto zimeonekana.
Aidha amewataka kusimamia suala la
kupeleka umeme kwenye taasisi kama vyuo, shule, makanisa, hospitali na
taasisi nyingine zikaweze kusaidia jamii ya maeneo husika.
Waziri Kalemani ametaja baadhi ya ajenda
moja wapo itakayojadiliwa katika kikao hicho ni utekelezaji wa
Sh.27,000 kupeleka umeme vijijini kwa nchi nzima.
“Kuna wateja wa kawaida wanalalamika
hawajaunganishiwa umeme miezi miwili au mitatu. mtu katoa pesa yake
analalamika tu lazima tukubaliane hapo tukarekebishe na kufikisha umeme
katika maeneo yaliyotengwa kwa ajiri ya uwekezaji” amesisitiza
Pia amesema miradi ya REA inayoendelea
kusuasua, ipo inayosuasua, inayokwenda kwa wastani na kwa kasi na
wakandarasi wanaoshindwa kufanya kazi tufanye nini, lazima tuchukue
hatua kama sereikali.
Amebainisha kuna miradi ya REA awamu ya
tatu, mpango wa raundi ya pili uko wapi nani analazimika kufanya nini
mpaka sasa kimpango ilitakiwa kuanza julai mwaka huu lazima tujue
tunajipanga hilo kwa namna gani.
Aidha Waziri amesema kuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya mameneja na wateja lazima mbadilike.
Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya
Nishati Dk. Hamis Mwinyimvua, amesema kuwa kikao hichi ni kwa ajili ya
kupeana maelekezo ya kazi, mahali pa kurekebisha na mahali pa kuongeza
bidii.
0 comments:
Post a Comment