NA
VERONICA MWAFISI, MOHA
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (pichani) amepokea ripoti mbili za uchunguzi ikiwemo
ya kifo chenye utata cha Isululu Kabote (85), mkazi wa Kijiji cha Buhungukila,
Kata ya Bugarama, Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu.
Kabote
alidaiwa kuuawa akiwa mikononi mwa polisi Mei 17, mwaka huu, saa 8:00 usiku. Pia
Lugola alipokea ripoti ya uchunguzi wa tukio la kutoroka mahabusu 17, Mei 21,
mwaka huu, mkoani Geita.
Mahabusu
hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita wakikabiliwa na
mashtaka mbalimbali na kuwekwa kwenye Ukumbi wa Jengo Jipya la mahakama
wakisubiri kusomewa kesi zao.
Ripoti
ya uchunguzi wa kifo cha marehemu Kabote iliwasilishwa na Lalph Meela (Mwenyekiti),
kutoka Dawati la Malalamiko Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wajumbe
ni Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Ibenze Ernest,
Kefa Kaswamila kutoka Dawati la Malalamiko Kitengo cha Upelelezi Wizara ya
Mambo ya Ndani na Mzee Mzee kutoka Ofisi ya Ofisa Usalama, Mkoa wa Simiyu.
Kamati
hiyo ilifanya uchunguzi huo kuanzia Juni 4-10, mwaka huu ambapo ripoti ya
uchunguzi wa tukio la kutoroka wafungwa ilikabidhiwa na Mwenyekiti wake, Alex Mfungo.
Baada
ya kupokea ripoti hizo, Lugola alisema ameridhishwa na matokeo ya uchunguzi huo
ambapo wajumbe wa kamati zote walipata fursa ya kuzichambua ripoti hizo
sambamba na kutoa mapendekezo.
Viongozi
wengine waliokuwepo wakati Lugola akipokea ripoti hizo ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima.
Kamati
ya uchunguzi wa kifo cha Kabote iliundwa baada ya wananchi wa kijiji hicho
kudai kabla ya kukumbwa na mauti, alikamatwa na polisi, kupigwa akidaiwa hajatoa
mchango wa maendeleo sh. 50,000 madai ambayo Jeshi la Polisi liliyakanusha.
Mmwili
wa marehemu Kabote ulikaa siku 20 katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili
ya uchunguzi wa kidaktari.
0 comments:
Post a Comment