METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 21, 2019

MISRI YAANZA VYEMA AFCON 2019,YAICHAPA 1-0 ZIMBABWE

Trezeguet (wa pili kushoto) akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Misri ikiilaza Zimbabwe 1-0

……………

WENYEJI, Misri wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe usiku wa Ijumaa Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mahmoud Ibrahim Hassan maarufu kwa jina la utani, Trezeguet anayechezea klabu ya Kasımpasa ya Uturuki aliyefunga dakika ya 41 akimalizia pasi ya beki wa Al Ahly ya nyumbani, Ayman Ashraf .
Matokeo hayo yanamaanisha kikosi cha kocha Mmexico, Javier Aguirre Onaindia kinaanza vyema kuwania taji la nane la AFCON baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.
Mshambuliaji ws Liverpool, Mohamed Salah aliwekewa ulinzi mkali na wachezani wa Zimbabwe kiasi cha kushindwa kufurukuta leo.
Kesho kutakuwa na mechi mbili, ya Kundi A Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Uganda kuanzia Saa 11:30 itakayofuatiwa na za Kundi B Nigeria dhidi ya Burundi Saa 2:00 usiku na Guinea na Madagascar Saa 5:00 usiku.
Taifa Stars itatupa kete yake ya kwanza jumapili kwa kumenyana na Simba wa Teranga kuanzia Saa 2:00 usiku, itakayofuatiwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Algeria na Kenya Saa 5:00 usiku, ambazo zitatanguliwa na mechi ya Kundi D kati ya Morocco na Namibia Saa 11:30 jioni.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com