Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akipata maelezo kuhusu kilimo
shadidi kutoka kwa mtaalamu wa Kilimo Dkt Kisa Kajigili
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Mkoani humo kujionea hmaandalizi ya maonesho ya Nanenane.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongozana na mtaalamu kutoka wizara ya Kilimo Dkt Kisa Kajigili wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya maonesho ya Nanenane.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Simiyu
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni 2019
alitembelea Viwanja vya Nyakabindi vilivyopo Mkoani Simiyu kujionea maandalizi ya
maonesho ya Wakulima (Nanenane) ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti 1-8 katika
maeneo mbalimbali nchini.
Akiwa
katika viwanja vya Nyakabindi Katibu Mkuu huyo alijionea maeneo mbalimbali likiwemo
eneo la Wizara ya Kilimo na kujionea vipando vya mazao mbalimbali ambavyo
vimefikia hatua nzuri.
Akizungumza
na maafisa wa wa Wizara ya Kilimo sambamba na maafisa wa Mkoa wa Simiyu
Mhandisi Mtigumwe alisisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kuandaa vipando vya
mazao yote yenye tija kubwa ikiwemo
Matunda na mboga mboga.
Kadhalika
alisisitiza kuongezwa kasi ya maandalizi ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaagiza
Maafisa hao kufanya maandalizi mazuri yatakayokuwa Mfano kwa wadau wengine.
Aidha,
baada ya kutembelea viwanja hivyo Mhandisi Mtigumwe alikutana na mwenyeji wake
ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka ambapo walifanya mazungumzo
kuhusiana na shughuli za Kilimo katika mkoa wa Simiyu.
Baada
ya Ziara hiyo katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita na Simiyu Mhandisi
Mtigumwe amerejea Jijini Dodoma kuendelea na shughuli zingine.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment