
*******************
Katika kuunga mkono na kuieleza
jamii juu ya juhudi zinazofanya nwa serikali ya Awamu ya Tano chini ya
Uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya
Sumbawanga Kiheka Charles a.k.a K Chars ameibuka na wimbo wa kuelezea
mazuri yanayofanywa na serikali ya Tanzania.
Katika kueleza malengo ya kutunga
wimbo huo alioupa jina la Mchaka Mchaka na kumshirikisha msanii Mackpaul
Sekimanga a.k.a Makamua, K Chars alisema kuwa kama kiongozi na mshauri
wa wasanii ni jukumu lake kuwaonesha wasanii mada mbalimbali za kuimba
na sio kujikita kuyaimbia mapenzi wakati wanaweza kuimba kuhusu
kuhamasisha lishe bora, kuhimiza kilimo cha mazao mbalimbali na faida
zake, kukemea mimba za mashuleni, ndoa za utotoni, kuboresha huduma za
afya nakadhalika.
“Hakuna msanii wa nje atakayekuja
kusifu nchi yetu isipokuwa sisi wenyewe kusifia maendeleo yetu na
kuyatangaza kwa wengine, hivyo nikaona niyaweke katika wimbo mazuri
yaliyofanywa na serikali ambayo jamii inapaswa kuyafahamu, msanii ana
nafasi kubwa ya kusikilizwa na jamii na yapo mengi ya kuyazungumzia
katika maisha yetu, hivyo ni vyema wasanii wakajielekeza katika
kuhamasisha mambo ya kimaendeleo, kuyaimba mazuri ya serikali na
kuyaibua yale ambayo wanaona serikali inahitaji kuyafahamu ili yafanyiwe
kazi,” Alisema
Halikadhalika, alisifu juhudi za
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, James Mtalitinya, kwa kumuunga
mkono katika juhudi za kuibua vipaji vya wasanii wa Sumbawanga tangu
kuanzishwa shindano la “Sumbawanga Talent Search” lililowahusisha
wasanii wa kuimba, hadi kumalizika kwa shindano hilo.
Katika Shindalo hilo ambalo
fainali yake ilifanyika usiku wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2019 na
mshindi wa kwanza alipata shilingi 300,000/=, wa pili 200,000/= na wa
tatu 100,000/= na walioingia kwenye kumi bora wamepewa fursa ya kurekodi
wimbo wa kuelezea fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa wa
Rukwa pamoja na kusifu ukarimu wa watu wa mkoa huo, kibao
kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi July,2019.
K Chars ametumia fursa hiyo
kuwaomba viongozi mbalimbali wa mkoa kuwasaidia na kuwaunga mkono
wasanii wachanga wanaoutangaza mkoa.
0 comments:
Post a Comment