Na Subira Kaswaga (Afisa Habari NEC)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imefanya uteuzi wa Madiwani Wanawake wa Viti Maalum saba (07) katika
Hamlashauri za Manispaa za Sumbawanga na Tunduma, Halmashauri za Wilaya
za Tandahimba, Korogwe na Rombo.
Akizungumza ofisini kwake jijini
Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk
amesema kuwa, uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka
kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa juu ya uwepo wazi wa
nafasi za Madiwani Wanawake wa Viti Maalum katika halmashauri hizo
kutokana na sababu mbalimbali.
Amezitaja sababu hizo kuwa ni
pamoja na waliokuwa Madiwani katika Halmashauri hizo kufariki dunia,
kujiuzulu na kuvuliwa uanachama na hivyo nafasi zao kuwa wazi.
Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk
amewataja Madiwani walioteuliwa na vyama wanavyotoka kuwa ni Regina
Willbard Lyakurwa na Beatrisi Revocatus Silayo Halmashauri ya Wilaya ya
Rombo, Regina Abiudi Liffi Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na
Agness Atanazi Chilulumo Halmashauri ya Manispaa ya Tunduma wote
wanatoka CHADEMA.
Wengine ni Shahara A. Alfani na
Mey R. Dadi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kutoka CUF na Mwajuma
Waziri Kitumpa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kutoka CCM.
0 comments:
Post a Comment