Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akiongea machache
wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa
vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei
22, 2019Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama
Janeth Magufuli, akiongea machache wakati wa hafla ya kutoa
msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye
uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimsiliza Katibu
Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma akitoa shukurani wakati wa kutoa msaada
wa vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji
jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi Katibu
Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Muma msaada wa vyakula kwa ajili ya futari
kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo
Jumatano Mei 22, 019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi
Mkurugenzi wa Hija wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile msaada wa vyakula
kwa ajili ya futari kwa niaba ya vikundi mbalimbali vyenye uhitaji
jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 22, 2019
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli katika picha ya
kumbukumbu na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu Mruma, Mkurugenzi wa
Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile pamoja na wawakilishi wa
vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji baada ya hafla ya kutoa msaada wa
vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, akimkabidhi mmoja
wa wawakilishi msaada wa vyakula kwa ajili ya futari kwa niaba ya
vikundi mbalimbali vyenye uhitaji jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei
22, 2019
…………………………………………………..
Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli, amewasihi Waislamu
nchini kuendelea kuliombea Taifa muda wote, hususan katika kipindi hiki
cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kuendeleza mshikamano bila
kujali dini ama kabila tabaka zao.
Mama Magufuli ametoa wito huo leo
tarehe 22 Mei, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa
vyakula kwa ajili ya futari kwa vikundi mbalimbali vyenye uhitaji.
Vyakula alivyotoa ni tani 5 za mchele, tani 3 za sukari na tende.
Hafla hiyoimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA Shekhe Nuhu
Mruma, Mkurugenzi wa Hijja wa BAKWATA Shekhe Haidary Kambwile na
wawakilishi wa vikundi mbali mbali vya wenye uhitaji.
Mama Magufuli pia amemuomba
Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, azikubali funga za Waislamu wote na
kuwalipa malipo stahiki wakati wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za Dini
ya Kiislamu.
“Kipindu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kipindi cha toba. Ni
kipindi cha kutenda matendo mema na kujizuia na vitendo viovu” amesema Mama Magufuli.
Mama Magufuli amesema licha ya
kwamba Tanzania ina watu wa imani za Dini tofauti lakini siku zote
wananchi wake wamekuwa wakishirikiana nyakati za dhiki na za raha bila
ubaguzi.
Ametoa mfano kuwa licha ya tofauti za kidini zipo baadhi ya familia
ambazo Baba Muislamu na Mama ni Mkristo zinaishi kwa amani na
kushirikiana katika masuala yote ya kifamilia na kwamba sifa hii ni
moja nguzo muhimu za umoja wa Watanzania.
“Binafsi nakumbuka zamani nikiwa
mdogo tulikuwa tunatafuta Mwislamu aje atuchinjie kuku ama mbuzi ama
ng’ombe” , alisema na kuongezea: “Ni kutokana na utamaduni huo
uliojengeka miongoni mwa Watanzania , leo nimeguswa kutoa sadaka yangu
kwa ajili ya ndugu zangu wenye uhitaji…”
0 comments:
Post a Comment