Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa neon la
ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji wa Uingereza nchini
alipokutana nao Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach
Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
Balozi
wa Uingereza Nchini, Mhe. Sarah Cooke akizungumza jambo wakati wa
mkutano wa wawekezaji wa nchi hiyo walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipokutana nao Jijini
Dar es Salaam.Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde
akichangia jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari
walipokutana kujadili masuala ya wawekezaji nchini Jijini Dar es
Salaam.Katikati ni Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo anayeshughulikia
Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa
Uingereza Nchini Mhe. Sarah Cooke.Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Bi. Oliver Vengula akichangia hoja wakati wa mkuatano huo.Kamshina
wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Gabriel Malata akichangia hoja
kuhusu vibali vya ajira wakati wa mkutano wa wawekezaji wa Uingereza
uliofanyika Jijini Dar es Salaam.Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bw. Russell Stuart akiuliza swali wakati wa Mkutano huo.Kaimu
Mkurugenzi wa Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Aristides Mbwasi akijibu
hoja za wajumbe kuhusu masuala ya uwekezaji wakati wa mkutano huoWaziri
wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
(Mb)akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchine Mhe. Sarah Cooke wakati
wa mkutano huo.Sehemu
ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi – Ofisi
ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani)
wakati wa mkutano huo.Mkurugenzi
wa Uhamasishaji Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. John
Mnali akiwasilisha mada ya fursa za uwekezaji nchini wakati wa mkutano
huo.Waziri
wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Kazi,
Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati wa Mkutano huo.Waziri
wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mahojiano
kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
……………………….
MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria kuendelea kutatua
changamoto zinazowakabili wawekezaji nchini ili kuhakikisha kunakuwa na
mazingira rafiki yatakayowavutia kuwekeza nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki
wakati akifungua mkutano wa wawekezaji wa Uingereza waliopo nchini
walipokutana kujadili masuala ya Uwekezaji uliofanyika Mei 29, 2019
katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira
Mhe.Anthony Mavunde, Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke pamoja
na Mwenyekiti wa Makampuni ya Biashara ya Uingereza Bw.Kalpesh Mehta,
viongozi wa makampuni ya uwekezaji nchini, pamoja na baadhi ya viongozi
wa Taasisi za Sekta ya Umma na Binafsi.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri
Kairuki alieleza lengo la kukutana na wawekezaji kutoka Uingereza ni
pamoja na kujadili masuala yote yanayowahusu wawekezaji kwa kuzingatia
changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzitatua ili kuendelea
kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya biashara na uwekezaji
nchini.
“Tumezingati umuhimu wa wawekezaji
nchini, hivyo tumekutana hii leo ili kusikiliza kero na changamoto
zinazowakabili ili kuona namna bora ya kuboresha mazingira na kutambua
fursa zilizopo nchini ili kuendelea kuwekeza nchini”, alisema Waziri
Kairuki.
Waziri aliongezea kwamba, kwa kuzingatia
kuwa mnamo mwezi Machi mwaka 2019 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aliutangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa
uwekezaji alipokutana na waheshimiwa mabalozi wa nchi za nje ambao wapo
nchini ikiwa ni kiashiria cha kufungua mwaka mpya.
Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia mchango
wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo ongezeko la ajira hivyo
tunapaswa kuzingatia na kuboresha mazingira yatakayochochea kuendelea
kuchangia katika uzalishaji wa ajira nyingi nchini.
“Sekta binafsi ndiyo kiini cha ukuaji wa
uchumi kwa upande wa kuongeza ajira hivyo tunatambua mchango huo ambapo
hadi sasa wawekezaji wa uingereza wamechangia katika ukuaji wa ajira kwa
kuzalisha ajira laki tatu,”alisisitiza Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza
Nchini Mhe.Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuona
umuhimu wa kukutana pamoja kujadili masuala ya uwekezaji na kuendelea
kujadili namna ya kuwezesha wawekezaji kutoka uingereza kuendelea kuwa
wadau muhimu nchini na kuhakikisha nchi zote mbili zinanufaika.
“Ni kweli tumeenedelea kuwekeza Tanzania
kwa kuzingatia mazingira yaliyopo hivyo ni vyema kukawa na maboresho
zaidi katika mazingira hayo kwa kuendelea kutatua changamoto zilizopo
kwa sasa ili tuendelea kushirikiana pamoja,” alieleza Balozi.Cooke
Aliongezea kuwa nchi ya Uingereza
imelenga kuwa kinara cha uwekezaji katika nchi za Afrika hiyo ni wakati
sahihi wa kuendelea kutumia fursa zilizopo barani humo ili kufikia
malengo.
“Ifikapo mwaka 2022 Nchi yetu imeweka
malengo ya kuwa wawekezaji bora barani Afrika hivyo tunaendelea
kushirikianana nchi za Afrika ili kuwa na nia moja na kuwa na mahusiano
yenye tija hasa katika masuala ya uwekezaji”,alisema Balozi Cooke.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde
alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili
kuchangia ongezeko la ajira kwa vijana wa Kitanzania ili kujikwamua
kiuchumi.
Aidha alifafanua kuwa, ili kuendelea
kukuza ujuzi kwa vijana na kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira
Serikali itaendelea kulinda ajira za watanzania na kuboresha mazingira
ya sekta binafsi ambao ni wadau muhimu katika kuzalisha ajira nchini.
0 comments:
Post a Comment