METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, April 24, 2020

ZANTEL YAZINDU A OFA KABAMBE YA MSIMU HUU WA MFUNGO WA RAMADHAN

Meneja Uhusiano wa Zantel Rukia Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofa maalum ya mfungo wa Ramadhani jijini Dar es salaam, Ofa hiyo mpya itawapa wateja uhuru zaidi wa kuwasiliana pamoja na kuwapa taarifa muhimu kipindi cha mfungo kama nukuu za Quran pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala kufuturu na mwisho wa kula daku.

Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel April 23, 2020 imezindua ofa maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake ili kuwawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zenye kujenga imani zao katika mwezi huu mtukufu.

Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na kupata taarifa muhimu kama vile nukuu mbalimbali za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala na ujumbe wa sauti utakaoingia kwenye simu zao kama simu nyakati za iftar na nyakati za daku.

Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa alisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha mfungo.

“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii itahakikisha kwamba wateja wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.

Naye, Meneja bidhaa na huduma wa Zantel, Aneth Muga alisema ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi vilivyoboreshwa zaidi vya siku,wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.

“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema Muga.

Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi 2,000 mteja atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata dakika 1,250, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu, jumbe za kuwakumbusha muda wa kufuturu pamoja za kukumbusha muda wa swala. 

Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na kuchagua namba 1 ambayo ni Ramadhani ofa na atajiunga na kifurushi anachohitaji.

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.

Aidha,Miundombinu hiyo imeiwezesha Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com