Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiongea wakati akikagua shamba darasa la zao la chai alipotembelea Chuo Kikuu cha Sokoine leo mjini Morogoro.Kulia kwake ni Dkt.Kudra Abdul Mkuu wa Idara ya Mimea Vipande na Kilimo cha Bustani.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiongozana na Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine Prof.Raphael Chibunda (kulia) kukagua miradi ya chuo hicho leo mjini Morogoro
Wakurugenzi wa Idara toka wizara ya Kilimo wakiwa kwenye kikao na Menejimeti ya Chuo Kikuu cha Sokoine na kujadili ushirikiano wa kuongeza tija na uzalishaji mazao nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika mche wa nanasi wakati alipokagua shamba darasa la kufundishia wanafunzi chuo Kikuu cha Sokoine leo mjini Morogoro.Kushoto ni Bw.Ramadhani Omari Mhadhiri wa mafunzo ya bustani na wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA Prof.Raphel Chibunda.
ya Kilimo imekubaliana na Chuo Kikuu cha
Kilimo Sokoine kuanza kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo ili kujitosheleza
na mahitaji ya wakulima nchini.
Makubaliano hayo yamebainishwa leo (24.04.2020)
na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alipokutana kwa mazungumzo na
Menejimenti ya Chuo hicho mjini Morogoro na kueleza kuwa nchi bado
haijajitosheleza na mbegu bora.
“Tunahitaji ushirikiano wa kuzalisha mbegu bora
za mazao ya kilimo kwa wingi ndani ya nchi ili kukidhi mahitaji ya wakulima ”
alisisitiza Katibu Mkuu
Wizara
ya Kilimo inapenda chuo Kikuu cha Sokoine
kianzishe vitalu vya uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga mboga na
matunda ili kupunguza utegemezi toka nje ya nchi.
“Ifike hatua nchi yetu kuwa na uhakika wa mbegu
bora na hai.Hii itaongeza ajira kwa vijana na wakulima kupata manufaa” alisema
Katibu Mkuu Kusaya
Kusaya alitaja maeneo mengine ya ushirikiano na
Chuo Kikuu cha Sokoine kuwa ni kuanzisha
maabara bora ya kilimo ili kusaidia mapinduzi katika utafiti,uanzishwaji wa
mashamba darasa kwa wahitimu wa masomo ya kilimo na kujenga maabara ya kisasa
ya kupima ubora wa mazao yakiwemo mboga mboga na matunda kabla ya kusafirisha
nje ya nchi ili kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
Pia uhamasishaji matumizi ya teknolojia ya bora
ya uzalishaji kwa kutumia zana za kisasa na utoaji huduma za ugani na mafunzo
ya muda mfupi kwa wataalam wa wizara na
wakulima kwa kutumia vyombo vya habari na TEHAMA ,Ili kuwa na kilimo chenye tija na manufaa kwa
mkulima ,Katibu Mkuu Kusaya amekiomba chuo cha Sokoine kusaidia jitihada za
wizara kudhibiti visumbufu vya mimea na mazao kama viwavijeshi,ndege waharibifu
wa kwerea kwerea,nzige wa jangwani,panya na magugu yanayoathiri mazao ya
wakulima.
“Tunahitaji sifa nzuri ya ubora wa mafunzo na
wataalam wa chuo kikuu cha Sokoine
iendelee na kuwanufaisha wakulima kuongeza tija na uzalishaji kwa kudhibiti visumbufu vya mazao yake. “
alisema Kusaya ,Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya kilimo kuwa
uzalishaji wa ndani wa mbegu bora umefikia tani 61,703 mwaka 2019
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Kilimo Sokoine Prof,Raphael Chibunda alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea
chuo hicho na kuwa wapo tayari kuanzisha mafunzo maalum ya muda mfupi kwa ajili
ya kufundisha wataalam waliopo kazini na wale wanaopenda kujifunza kilimo cha
kisasa.
Prof.Chibunda alisema SUA itaendeleza
ushirikiano na Wizara ya Kilimo kupitia taasisi za utafiti wa Kilimo (TARI) na
kampuni ya mbegu nchini (ASA) na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Tanzaia (TOSCI)
kuzalisha mbegu bora za mazao kwa
kutumia teknolojia na wataalam waliopo nchini.
“SUA ina msitu wa wataalam hivyo tunaahidi
tutashirikiana na wizara ya kilimo kufanya tafiti za mbegu bora na pia
kuzalisha mbegu hizo kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. ” alisitiza
Prof.Chibunda
Aliongeza kusema kina mkakati wa kuanzisha
digrii maalum itakayosaidia kuzalisha wataalam wabobezi kwenye usimamizi wa
sekta ya ushirika na kilimo nchini ili kuunga mkono jitahada za serikali kuwa
na ushirika imara.
Katika hatua nyingine Prof.Chibunda aliomba
Serikali iweke utaratibu wa kuratibu waduka ya pembejeo ili yawe na wataalam
waliosomea kilimo na mifugo kwa ajili ya kutoa huduma za ushauri kwa wakulima.
Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo alisema
lengo la wizara yake ni kuhakikisha kunakuwepo sera nzuri na mazingira wezeshi
ya kufanya kilimo kuwa ajira, uchumi na biashara kwa watanzania walio wengi.
0 comments:
Post a Comment