Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo na Rais Mstaafu wa
Naigeria Olusegun. Obasanjo walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa
Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika
kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati
waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya
miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .mwenye Tai nyekundu akiwa na viongozi wa
mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 katika wakitoa heshima katika eneo la kumbumbu
ya mauji ya kimbari Waziri Mkuu yupo Kigali Rwanda akimuwakilisha Rais Dr
John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano ambavyo ni tunu walizoachiwa na
waasisi wa Taifa.
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Aprili 7,
2019) katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya Kimbari iliyofanyika katika
jiji la Kigali nchini Rwanda.
Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais
Dkt. John Magufuli katika kumbukumbu hizo, amewasisitiza Watanzania kudumisha
amani na utulivu.
Awali,Waziri Mkuu alijumuika
na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu ya
mauaji hayo la Gisozi lililopo jijini Kigali.
Baada ya kutoa heshima kwenye eneo la
kumbukumbu za mauaji hayo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitoa maelezo ya kina
kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Rwanda 1994.
Viongozi wengine waliohudhuria
kumbukumbu hizo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na
Rais Mstaafu wa Nigeria, Ulusegun Obasanjo.
0 comments:
Post a Comment