NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge,
Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka
waajiri wote nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na
usawa maeneo ya kazi.
Ameitoa kauli hiyo hii leo tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua
semina ya siku moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya
wafanyakazi nchini walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini
ikiwemo; haki na wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa
mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.
Waziri alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo
katika jamii ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi
yanayoweza kukwamishi jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni
viungo muhimu katika kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.
“Mchango wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika
nyanja zote za ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize
wajibu wao kwa kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na
waendelee kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi
wengine.”alisisitiza Waziri Mhagama.
Waziri alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema
sheria na taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na
waajiriwa wenye kuzingatia usawa wa kijinsia.
“Ninakemea vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo
kukoseshwa haki zao na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika
kukemea matendo hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.
Aidha Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya
wafanyakazi kama jukwaa maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.
Aliongezea kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana
budi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
yaliyopo katika masuala ya kazi.
“Wanawake umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili
kuwa na vigezo mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya
kazi.”alisisema Waziri Mhagma.
Naye rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini
Nyamhokya alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki
sawa kwa wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili
kuwasaidia wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao
ya kazi.
“Wanawake wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao
wawapo kazini ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza
Nyamhokya.
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea
kuchangamkia fursa za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake
vitakavyosaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la
uzalishaji nchini.
0 comments:
Post a Comment