Na Emmanuel Michael Senny, Kigoma
Wakulima katika halmashauri za Kasulu, Kibondo, Buhigwe na
Kakonko mkoani Kigoma wameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo, kutoa elimu
ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo pamoja na upatikanaji mbolea kwa
wakati ili kufanya kilimo chenye tija na kuunga mkono juhudu za serikali
kufikia uchumi wa kati.
Venansi Mseka na Manuni Mapuli ni baadhi ya wakulima hao ambapo
walisema licha ya serikali kuweka mikakati ya wakulima kupata mbolea kwa wakati
changamoto ya upatikaji elimu bado ni kitendawili ambapo mbolea hiyo imekuwa
sehemu ya kuharibu mazao kwa kile wanachodai kutumika bila kuzingatia elimu.
"Mbolea tunaweza kuzipata kwa wakati, lakini shida kubwa ni
namna ya kuzitumia, wengi wetu hatujui matumizi sahihi ya mbolea hizi ndio mana
licha ya kuwa tunaweka mbolea kwenye mazao ila bado tunapata hasala wakati wa
mavuno, hivyo tusaidiwe elimu zaidi ili kunusuru kilimo chetu" walisema
Wakulima hao.
Hayo yameelezwa mara baada ya kupatiwa elimu kwa wakulima wa
halmashauri hizo na kampuni ya GSM katika utambulisho wa mbolea ya kampuni hiyo
ambayo inalenga kumfanya mkulima kulima kilimo chenye tija.
Kwa upande wake mkaguzi wa mbolea mkoa wa Kigoma Bw.Jakison
Kahabi amesema mkoa wa Kigoma unambolea ya kutoasha nakuwataka wakulima
kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea huku mhandisi wa kilimo na umwagiliaji
mkoa wa Kigoma Yohana Zefania akibainisha hatua za matumizi bora ya pembejeo
kupitia maafisa ugani kuwa watawafikia wakulima kwa wakati.
"Tumetoa kipaumbele katika utoaji wa elimu hivyo kwa
kuwatumia maafisa ugani ambao watakuwa wakiwatembelea wakulima mashambani
tunaamini wilaya zote mkoani Kigoma zitanufaika na kuanza kufanya kilimo chenye
tija" alisema Kahabi.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment