Na EMMANUEL MICHAEL SENNY, KIGOMA
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanal Marko Ngayalina
pamoja na na kamati ya ulinzi na usalama, wameungana na wananchi wa
kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani humo kupanda miti elfu 1000 katika
vyanzo vya maji ili kuimalisha upatikanaji wa maji Safi na salama katika vyanzo
hivyo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasumo mara baada ya zoezi
la upandaji wa miti Kanal Ngayalina aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji
ili waendelee kunufaika na huduma ya maji kijijini humo.
"Miti hii itasaidia kulinda vyanzo hivi ambapo wananchi
hamtakuwa mkipata shida ya maji kutokana na kukauka kwa vyanzo hivi, cha msingi
ni kuitunza miti hii " alisema Ngayalina.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kasumo Damasi
Gaburiel alisema wananchi wamekuwa wakihangaika kwa mda mrefu kutafuta maji, na
kwamba hatua hiyo itakuwa suluhisho la tatizo la maji kwa wananchi.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walimpongeza mkuu wa
Wilaya kwa namna ambavyo aliwahamasisha kupanda miti ili kumaliza tatizo
la maji kwa wananchi.
"Ni jambo la kujivunia kwa kiongozi wetu kuja kushirikiana
na wananchi wake katika shughuli za maendeleo, na hapa ni sisi wananchi ndio
tunanufaika kitakapofika kipindi Cha mito kukauka hatutakuwa na hofu kutokana
na miti tuliyopanda" walisema wananchi hao.
Mradi wa maji katika kijiji cha Kasumo umeghali zaidi ya milioni
306 ikiwa ni hatua ya pili ya kuimarisha mradi wa kijiji na wananchi kuendelea
kupata maji safi na salama pamoja na kumtua mama ndoo kichwani.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment