Na
Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) Gairo
Wachimbaji
wa Madini ya Rubi wilaya ya Gairo kata ya Iyombe kijiji cha Kirama, wamekimbia
na kutelekeza Madini ya viwandani aina ya Rubi Nut, Pikipiki na vifaa
mbalimbali vya kuchimbia baada ya kuona msafara wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini
Prof. Idris Kikula na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambae pia ni Mkuu wa
Wilaya (DC) ya Gairo Seriel Shaid Mchembe waliokuwa wanatembelea mgodi huo
kuona shuguli za uchimbaji kwa lengo la kwenda kutatua kero zinazowakabili.
Msafara
wa mwenyekiti wa Tume ya madini akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume hiyo Dkt.
Athanas Machiyeke na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ulianza majira
ya saa tatu asubuhi kuelekea kwenye eneo
la mgodi.
Wakiwa
njiani msafara huo ulikubwa na changamoto baada ya gari ya Polisi iliyokuwa
inaongoza msafara huo kukwama kwenye maji katikati ya mto kwa muda wa saa moja
kitendo kilichopelekea kuchelewa kufika kwenye eneo la mgodi.
Hata
hivyo mara baada ya kufika kwenye nyumba ya mchimbaji mmoja alie tambuliwa kwa
jina la Sadick Athuman maarufa kwa jina la (Saadam) alikutwa kijana mmoja aliejitambulisha
kwa jina la Athumani mkazi wa Gairo mjini akilinda mahali apo ndipo mkuu wa
Wilaya na vyombo vyake vya ulinzi na Mwenyekiti wa Tume na Kamishna waliingia
ndani na kufanya msako na kukuta madini aina ya Rubi Nut yakiwa kwenye mifuko,
Pikipiki moja na vifaa mbalimbali vya kuchimbia.
Alipo
ulizwa bwana Athumani, nani anae miliki madini hayo, alisema ni madini ya bwana
Saadam. Alipo ulizwa yeye anafanya nini alisema yeye ni kibarua tuu na mwenyewe
Saadam yupo mgodini anaendelea na uchimbaji ndipo Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama akamuamuru Athumani kwenda nae mpaka anakochimba bwana Saadam
na mara baada ya kufika eneo la mgodi wachimbaji wote wakakimbia na kuelekea
vichakani akiwemo bwa Saadam huku vifaa vya uchimbaji vikiwa vimetelekezwa
sambamba na madini yale ya kwenye mfuko na pikipiki.
Kufuatia
kitendo hicho mwenyekiti wa tume ya Madini Prof. Kikula amesikitishwa na
kitendo hicho ambacho kinaashiria uchimbaji wa mgodi huo unafanyika bila
kufuata sheria.
Kutokana
na hali hiyoo, mwenyekiti wa tume amemuagiza afisa Madini Mkazi mkoa wa Morogoro
Mhandisi Emmanuel Shija kufuatilia uhalali wa eneo hilo (Leseni na Codinates)
na mwenendo mzima wa uchimbaji wake, endapo eneo hilo litakuwa na leseni mmiliki
wake alipe maduhuli yote anayotakiwa kulipa tangu alipoanza na kama eneo hilo
halijakatiwa leseni mgodi huo ufungwe mara moja na shuguli za uchimbaji
zisitishwe mara moja.
Aidha,
amesikitishwa na wachimbaji na wawekezaji katika eneo hilo kushindwa kusaidia
shuguli za maendelo ya kijiji kinacho zunguka migodi hiyo ambapo ofisi yake
haikumridhisha mwenyekiti wa tume.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo amesikitishwa na wachimbaji hao kwa kukiuka
sheria zinazo ongoza shuguli za uchimbaji madini, amesema amekuwa akiwahimizi
mara kadhaa wachimbaji wote wilayani humo kuzingatia na kufuata taratibu kabla
hawajanza kazi za uchimbaji ikiwemo kukata leseni na kulipa maduhuli ya
serikali.
Kufuatia
kwa tukio hilo Mchembe amepiga marufuku kwa mtu yeyote katika wilaya ya Gairo
kufanya shuguli za madini bila kuwa na kibali kutoka tume ya madini.
Wakati
huo huo Mchembe amemuagiza Kamanda wa Polisi wilaya ya Gairo Lugano Piter Mwakisunga
kuhakikisha anamkamata Sadick Athumani ndani ya siku saba na kumfikisha kwenye
vyombo vya sheria.
Wakiwa
kwenye mgodi wa eneo la mwekezaji wa kampuni ya Mofar Holdings (T) Ltd Kamishna
wa Tume ya Madini Dkt. Machiyeke amemsisitiza mwekezaji huyo kuzingatia
taratibu na sheria katika hatua ya kuajiri wafanyakazi na vibarua na manunuzi
ya bidhaa kama muongozo unavyo sema.
Dkt.
Machiyeke amesema, sheria inasisitiza kutoa kipaumbele kwa wananchi waozunguka
mgodi na taifa kwa nafasi kubwa kabla ya kufikiria nje ya eneo hilo na nje ya
nchi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Madini na Kamishna walikuwa wanahitimisha ziara yao ya siku tano
katika mkoa wa Morogoro baada ya kutembelea wilaya ya Morogoro mjini, Ulanga,
Mvomero na Gairo ambapo ujumbe wake mkubwa kwa wafanyakazi wa tume na
wachimbaji madini ulikuwa ni uadilifu katika kazi zaona kuepuka rushwa.
0 comments:
Post a Comment